Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 2, 2016

Mitumba kupigwa marufuku Afrika Mashariki

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana leo mjini Arusha, Tanzania wameamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo na vitu vikuu vya mitumba. Utekelezaji wake utakuwa baada ya miaka mitatu. Marufuku hiyo ni moja ya hatua zilizopendekezwa ilikuinua viwanda vya nguo katika kanda ya Afrika Mashariki. Serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikilaumu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira. Nguo. Nguo hizo hutegemewa sana na watu wenye mapato ya chini kutokana na bei yake nafuu. Kadhalika, wauzaji wa nguo hizo wasafirishaji,waagizaji wote huzitegemea kupata mkate wao wa kila siku hii ikichangia pato la nchi na ajira kwa maelfu ya watu ambao huhudumu katika biashara hiyo. Viongozi hao pia watajadili pendekezo la kupunguza kiasi cha magari yaliyotumika yanayoingizwa kanda hii. Lengo lao likiwa kutafuta mbinu ya kusaidia viwanda vya utengenezaji magari vinavyoendesha biashara Afrika Mashariki. Maombi ya Sudan Kusini na Somalia kutaka kujiunga na jumuiya hiyo pia yalijadiliwa. Sudan Kusini ilikubaliwa kujiunga kama mwanachama wa 6 wa muungano wa mataifa ya Afrika Mashariki. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wanatarajiwa kuzindua pasipoti ya pamoja ya Afrika Mashariki ambayo itakuwa katika mfumo wa elektroniki.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment