Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 16, 2016

Rais Magufuli asema hasara ya mishahara hewa inafikia billioni 2.5 kwa mwezi

Rais wa Tanzania John Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni nchini humo huku akizungumzia upotevu mkubwa wa mapato ya serikali unaotokana na kuwepo watumishi hewa Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu hao wa mikoa rais Magufuli amesema tatizo la wafanyakazi hewa limekuwa likigharimu serikali fedha nyingi, ambapo ametolea mfano wa uchunguzi uliofanywa katika mikoa miwili ya Dodoma na singida na kubaini takriban wafanyakazi hewa 202 katika halmashauri 14. Amesema kutokana na hali hiyo na ikichukuliwa taswira ya nchi nzima, hasara inayokisiwa inayotokana na malipo ya mishahara hewa ya wafanyakazi nchini Tanzania inafikia shilingi billioni 2.5 kila mwezi huku serikali ikitumia shilingi bilioni 549 kwa mwezi kwa ajili kulipa watumishi wake hivyo amewataka kuzisimamia vyema halmashauri zao. Wakuu wa mikoa wote 25 walioapishwa baadaye wamesaini kiapo cha uadilifu kilichosimamiwa na kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Salome Kaganda, huku makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwatahadharisha juu ya kusimamia vyema matumizi ya fedha za maendeleo. Rais Magufuli pia amewaapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru, Valentine Mlowola aliyewathibitisha kazini hivi karibuni baada ya kukaimu kwa muda nafasi hizo. VOA SWAHILI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment