Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 15, 2016

Majimbo 5 kuwateua wagombea urais Marekani

Majimbo matano nchini Marekani yanapiga kura kumteua mgombea atakayewania urais kupitia tiketi ya vyama vyao. Uchaguzi huo huenda ukawapa fursa wagombea wa vyama vya Democrat na Republican kuimarisha uongozi wao. Kura zimeanza kupigwa katika jimbo la Ohio na Florida yote yakionekana kuwa muhimu pamoja na majimbo ya Carolina Kaskazini ,illinois na Missouri. Mgombea wa chama cha Democratic aliye kifua mbele Hillary Clinton atatumai kwamba atafanikiwa kum'bwaga mpinzani wake wa karibu Bernie Sanders . Wakati huohuo Donald Trump atalenga kuwaangusha wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho. Bilionea huyo anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa mgombea wa Republican lakini anakabiliwa na upinzani katika chama cha Republican pamoja na chama cha Democrats. Aliandikisha ushindi wa mapema siku ya jumapili wakati aliposhinda wajumbe wote tisa katika kisiwa cha Kaskazini cha Mariana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment