Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 23, 2016

Obama amtaka Castro asiiogope Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama ameeleza matumaini yake kwamba hali ya Cuba itaimarika, kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga. Kiongozi huyo wa Marekani, ambaye ndiye wa kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo kutoka ukumbi wa Grand Theatre mjini Havana. Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama. Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa “usemi wa watu wa Cuba”. Obama na Castro wajibizana Cuba Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani na Cuba kuacha nyuma yaliyopita na kusonga mbele “kama marafiki na majirani na kama familia, pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi. Jumatatu, viongozi hao walijibizana kwenye kikao na wanahabari Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya kifalsafa na kujieleza sio kwa kupinga Marekani bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa Cuba. "Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na Wacuba ni Wacuba,” alisema. Aidha, amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana na raia wa Cuba. Ni Bunge la Congress pekee linaloweza kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo. Bw Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu kwa kuungana na Rais Castro kutazama mechi ya besiboli uwanja wa Baada ya kuondoka Cuba, Bw Obama ameelekea Argentina siku ambayo inalingana na maadhimisho ya miaka 40 tangu kutokea kwa mapinduzi yaliyoingiza mamlakani utawala dhalimu wa kijeshi. Baadhi ya makundi yanapanga maandamano kushutumu Marekani ambayo inadaiwa kusaidia jeshi wakati wa mapinduzi hayo ya 1976.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment