Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 22, 2016

Mabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar

Tume ya uchaguzi imesema asilimia 67.9 ya wapiga kura walijitokeza Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wamekosoa uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar Jumapili. Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein ametangazwa mshindi wa uchaguzi huo na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Chama cha Wananchi (CUF) kilisusia uchaguzi huo. Mabalozi wa Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Uhispania, Sweden, Uswizi, Uingereza na Marekani wamesema uchaguzi huo haukufaa kufanyika bila ya kuwepo kwa maafikiano kuhusu suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani humo. “Ili uchaguzi uwe wa kuaminika, ni lazima ushirikishe wote na uwe unaakisi nia ya watu,” mabalozi hao wamesema kupitia taarifa. “Tunakariri wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kutoa uongozi Zanzibar na kufanikisha suluhu kupitia mashauriano kati ya vyama, kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mabalozi hao walionekana kutoa wito kwa Rais John Magufuli kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo. Kiongozi huyo hata hivyo tayari amesema kwamba hataingilia mzozo katika visiwa hivyo. Shein Image caption Dkt Shein baada ya kupiga kura yake Bungi, Unguja Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na ZEC, Dkt Shein alipata kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4 ya kura zilizopigwa. Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohammed aliibuka wa pili na kura 9,734 (3.0%). Bw Seif Sharif Hamad wa CUF alipigiwa kura 6,076 (1.9%) licha ya kwamba chama chake kilisusia uchaguzi huo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment