Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 31, 2016

Aliyewakinga wakristo kutoka kwa al shabab atuzwa

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa. Rais Kenyatta alihutubia taifa Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi. Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab. Rais Kenyatta amemtuza Mwalimu Farah heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi. Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu. Al Shabaab: Wanawake waislamu waliwafunika Hijab wakristo Waislamu waokoa wakristo waliotekwa na al Shabab Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao. Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi. Kwa bahati mbaya Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja. Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab. Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa. Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu. Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment