Writen by
sadataley
3:21 PM
-
0
Comments
Marehemu Mandilindi William enzi za uhai wake akiwa jijini Nairobi nchini Kenya walipokwenda kihuduma na kwaya yake ya Neema gospel. |
Kwaya ya Neema Gospel ya kanisa la AIC Chang'ombe jijini Dar es salaam, imepata pigo la kuondokewa na mmoja kati ya wanakwaya wao aitwaye Mandindi William aliyefariki jana jioni katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wanakwaya wa kwaya hiyo kupitia ukurasa wa Facebook wa
Mandi kushoto akiwa na wapigaji wa Neema gospel. |
kwaya hiyo amesema wakati wakirekodi cd mpya ambayo wameizindua jumapili
iliyopita, kijana huyo aliwaambia wenzake kwamba anaumwa inni
akizungumza kwa utani ambao hata wenzake hao waliishia kucheka.
Marehemu Mandilindi alikuwa mmoja kati ya vijana watatu wa kwaya hiyo
ambao wanavipaji katika kuanzisha nyimbo akiwemo Samuel Limbu, Charles
Izengo pamoja na marehemu ambaye kupitia sauti yake ya upole ambayo
unaweza kuisikiliza kupitia wimbo wa 'Ponya kanisa lako' ulioimbwa na
kwaya hiyo ambapo kijana huyo anaimbisha kuanzia dakika ya 6 na sekunde
ya 22 akiimba 'Bwana ni nuru yetu nani tumhofu…' imewabariki wengi
waliosikiliza na kutazama wimbo huo.
Mandilindi wa kwanza kuume akiwa na wenzake ambao kwa pamoja walikuwa wakiitwa mapacha watatu kwa kazi yao njema katika kumuinua Kristo. |
Habari na Mtandao wa Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment