Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, June 30, 2013

WAANDISHI BHANA TUNABADILIKA KUTOKA NA UPEPO UNAPOELEKEA, TAZAMA HII KATUNI NA SOMA UJUMBE WAKE KWA MAKINI
  Picha kwa hisani ya  Gazeti la The Citizen

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA NA MAANDAMANO HUKO BRAZIL


Sepp Blatter
Rais wa Fifa Sepp Blatter, anaamini kuwa hadhi ya shirikisho la mchezo wa soka duniani imeimarika kutokana na fainali za kombe la shirikisho, inayoendelea nchini Brazil, licha ya maandamano yanayoendelea nchini humo.
Maandamano yanayoendelea nchini Brazil
Akiongea kwa mara ya kwanza, tangu maandamano hayo kuanza, Blatter amesema anawahurumia raia wa nchi hiyo wanaoandamana katika miji mia moja nchini Brazil.
Maandamano zaidi yanatarajiwa kabla ya fainali za kombe hilo siku ya Jumapili kati ya Brazil na Uhispania katika uwanja wa Marikani mjini Rio.
Kuna wasi wasi mkubwa kuwa huenda rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff huenda asihudhuria fainali hiyo.
'' Fifa imekuwa na nguvu zaidi na hadhi yetu imeimarishwa. Mchezo wa soka umekuwa na nafasi kubwa miongoni mwa taifa hili na imewapa fursa ya kuelezea hisia zao'' Alisema Blatter.
Blatter amesema anawahurumia sana raia wa nchi hiyo kwa kuwa anafahamu masuala wanayoyapinga kupitia maandamano hayo ya amani na ameongea kuwa anatarajiwa serikali ya nchi hiyo itatatua masuala hayo kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la dunia itakayoandaliwa nchini humo mwaka ujao.

Shirikisho la mchezo wa FIFA limeshutumiwa sana nchini Brazil kwa kupata faida kubwa isiyotozwa ushuru kutokana na fainali za kombe la dunia kuandaliwa nchini humo, na kuiacha taifa hilo kuwekeza mabilioni ya fedha za umma bila manufaa yoyote. Bwana Blatter hata hivyo amekanusha madai hayo.
''Dhamira kuu ya kombe la dunia sio kupata faida au kuchukua faida yote kutoka kwa nchi inayoandaa mashindano hayo, lakini ni kuisaidia taifa hilo ili kuhakikisha kuwa fainali hizo zinafanikiwa'' Alisema Blatter.
Blatter ambaye aliondoka nchini Brazil wiki iliyopita, huku maandamano hayo yakichacha, amepuuzilia mbali madai kuwa alitoroka Brazil hata bila kuwajulisha maafisa wengine wakuu wa Fifa.

Blatter amesema aliondoka Brazil ili kuhudhuria fainali za kombe la dunia kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 inayoandaliwa nchini Uturuki.

Kiongozi wa Al Shabaab ajisalimisha

 Hassa Dahir
Mmoja wa viongozi wakuu wa zamani wa kundi la wapiganaji wa Al-shabaab, Hassa Dahir Aweyes amewasili mjini Mogadishu chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya serikali.
Hata hivyo haijulikani iwapo kiongozi huyo amesalimu amri au ameamua kujiunga na vikosi hivyo vya serikali.
Ijumaa iliopita, umoja wa mataifa ulitangaza kuwa Bwana Hassa Dahir alikuwa amejisalimisha kwa vikosi vya serikali ya Somali lakini madai hayo yakapingwa na wazee wa koo za taifa hilo.
Kiongozi huyo alikuwa amechukua hifadhi katika mji wa Kazkazini wa Adado baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya kambi tofauti za wapiganaji wa Al Shabaab juma lililopita.
Kiongozi huyo ametajwa kama gaidi na umoja wa mataifa pamoja na serikali ya marekani.
RAIS  BARACK OBAMA   ATEMBELEA KATIKA GEREZA ALILOKUWA AMEFUNGWA RAIS MSTAAFU WA AFRIKA YA KUSINI MZEE NELSON MANDELA  HUKO KATIKA KISIWA CHA  ROBBEN
obama robben island
                     HUMU NDIMO ALIMOISHI MZEE NELSON MANDELA   AKITUMIKIA KIFUNGO CHA  MIAKA 18 

MZUNGU AKISAKATA MUZIKI WA INJILI WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA MITATU YA  KTUO CHA REDIO CHA KKKT- DAYOSISI YA IRINGA 

RADIO FURAHA  96.7FM JANA

Mmm hapa naona anaonesha umahili wake 
YUPO MAKINI SANA MTAZAME HAPA
 KWELI  KANISA LITAENDELEA KUWEPO DAIMA 
"YESU ANAUTAJIRI MKUBWA SANA"

Leo hii ni kilele cha Sikukuu ya Vijana kwa Usharika wa Kihesa  Dayosisi ya Iringa (KKKT)  hapa utaona ni sura za vijana, leo vijana walipewa nafasi kuonesha kama kweli wanaweza  kutumika katika  shamba la Bwana wetu Yesu Kristo. Kutoka kushoto ni  James Gasso, Ohard Mpesa, Happy Mdegella,Odiana Ngasakwa na mwisho ni  Eliud Nduye  na nyuma yao ni Mchungaji kijana kabisa Mchungaji Kurwa Sadataley 
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA 
DAYOSISI YA IRINGA

SIKUKUU YA VIJANA USHARIKA WA KIHESA 
JIMBO LA KASKAZINI 

NENO KUU : VIJANA NI KIU YA MABADILIKO KATIKA JAMII   

"SOTE TUKUBALI KUTUMWA KATIKA JAMII KWA HUDUMA MBALIMBALI TUNAZOITWA NA TULIZOITWA"-ISAYA  6:1-7


  Katikati ni Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchg. Donald Kiwanga, kushoto ni Mchg. Yusto Kinyoa na Mchg. Kisabugo
                                                                     Wazee wa kanisa wakiwa kazini
      Mkuu wa Jimbo akizungumza na vijana baada ya ibada ya Pili leo hii hapa katika Usharika wa Kihesa
                           Mchg. Yusto Kinyoa na Mchg. Kisabugo  mara baada ya Ibada ya pili
                                                  Wazee wa Kanisa Vijana wakiwa na Wachungaji

   
                             Wazee wa Kanisa wakiwa na Mchungaji Kijana   Mchg. Kurwa Sadataley
Wazee wa Kanisa Vijana wakiwa na Wachungaji
Ni wakati wa chakula  sasa






Sumaye: Vijana msikubali kununuliwa kwenye Uchaguzi

                                                                             Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye 
Na Pamela Chilongola na Benjamin Mwangoka, MwananchiDar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amewatahadharisha vijana kuwa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wasikubali kupewa rushwa ya kanga, fulana na fedha na mtu yeyote anayetaka kuingia madarakani.
Akizungumza jana alipokuwa kwenye bonanza la michezo la kikundi cha Ukwamani Jogging kilichopo Kawe, alisema vijana wawe makini katika kuchagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza ambaye atajali masilahi ya wananchi wake siyo kwa masilahi yake binafsi.
“Najiuliza kama ninajiamini nataka kugombea Kawe au Arusha au Sumbawanga kama ninafaa na wananchi wananiamini mimi ninafaa na wananchi wananihitaji kwa nini niwachochee kwa kanga au fedha ukiona hivyo huyo hawafai kuwaongoza,” alisema na kuongeza:
“Ukiona mtu anatoa kitu ili achaguliwe hafai kuwa kiongozi kwani uongozi ni mzigo,” alisema Sumaye.
Aliwashangaa watu wazima wanaochukua fedha na kuweka mfukoni kisha wanapita mitaani huku wakisema fulani anafaa kwa kuwa anatoa rushwa na fulani hafai kwa kuwa hatoi kitu chochote.
Sumaye alisema anayetoa fedha ili apewe kura huyo hafai kuwa kiongozi kwa sababu atakuwa anawatumikia watu wake waliompa fedha sio mwananchi ambaye alijitolea kumchagua kiongozi hiyo kwa kumpigia kula halali ili aweze kusaidia kumtatulia kero mbalimbali zinazomkabili.
Alisema kama kuna watu wanaumizwa kwa kuambiwa wanapokea au kutoa rushwa huku akiwa anaendelea na kufanya hivyo aache ili asiendelee kuumizwa na hilo.
Sumaye alisema nchi haiwezi kuwa na maendeleo kama viongozi wataendelea kudidimiza nchi kwa rushwa,ufisadi na kuingiza dawa za kulevya nchini.
Alisema viongozi wanaoleta dawa za kulevya kama ni nzuri wangezitumia lakini hawazitumii matokeo yake wanaoathirika ni vijana ambao wanategemewa kulijenga taifa hili.
“Hatuwezi kudidimiza jamii kwa kuwaletea dawa za kulevya ili watoto wa wenzao waharibikiwe kwa nini wasiwape au kutumia hao viongozi ili waathirike wao wenyewe?” alisema Sumaye

Saturday, June 29, 2013

Obama akutana na rais Zuma

Rais Obama na rais Jacob Zuma wakiwahutubia waandishi wa habari
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.
Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Ziara hiyo ya bwana Obama ina lengo la kuongeza mauhusiano ya kibiashara lakini imetekwa na hisia za ugonjwa wa bwana Mandela ambaye amelazwa hospitalini kwa muda wiki tatu sasa kutokana na maradhi ya mapafu yanayosumbua mfumo wake wa kupumulia.
Katika kikao hicho wawili hao walizungumza na vyombo vya habari kuhusu ushirikiano wa mataifa yao kibiashara mbali na kutafuta suluhu ya kudumu katika mataifa yaliokumbwa na ghasia mashariki ya kati.
Ikulu ya White House imesema kuwa Obama pia atakutana na familia ya Mandela anayeugua maambukizi ya mapafu ili kuifariji.
Awali Rais Obama, aliye ziarani barani afrika alitoa shukran za dhati kwa uongozi ulioonyeshwa na Mandela.
Wakati wa ziara hiyo Obama pia atakutana na wanafunzi huko Soweto kabla ya kuelekea katika jela la Robben Island ambayo Mandela alihudumia kifungo chake cha miaka 27 wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA IRINGA 
YAFANYA SEMINA ZA VIJANA KAMA SEHEMU YA  KUSHEREHEKEA SIKUUU ZA VIJANA 

HAPA NI LEO HII  KATIKA USHARIKA WA KIHESA  JIMBO LA KASKAZINI 

                    IMEFANYIKA KATIKA KITUO CHA VIJANA HAPA USHARIKANI
     PICHA YA  SEHEMU YA KANISA NA HAPA NI MWINJILISTI NESIA  MWILAFI  WA USHARIKA WA KIHESA 
                                                    VIJANA WAKIWA DARASANI







     MKUU WA JIMBO MCHUNGAJI DONALD KIWANGA AKIFUNDISHA  VIJANA
                         MWINJILISTI  SHEM   MSITE  KATIBU WA VIJANA USHARIKA
                            HAPA  WAKIWA KATIKA MAANDALIZI YA IBADA YA KESHO


KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI  TANZANIA 


DAYOSISI YA IRINGA 

"NAFASI YA KIJANA KATIKA KANISA".

SOMO LILOTOLEWA KATIKA KONGAMANO LA VIJANA  KATIKA USHARIKA  WA KIHESA 29-06-2013

Kanisa ni nini?
Kanisa  si jengo  tu bali ni wale waliomo ndani yake. Maana yake ya asili toka neno la Kiyunani ni ekklesia “kusanyiko”  "walioitwa" kama maneno katika msalaba ambao huwa ninauvaa. Neno Kanisa Iimo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."
Kanisa ni watu wanao amini Waefeso 2:21 "Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika bwana." 1Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.
Kazi ya kanisa ni ipi? Kanisa linaeneza ijili  2 Timotheo 4:2 "Lihubiri neno uwe tayari wakati ufaao na wakati usiokufaa karipia kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."
Kanisa limepewa maagizo na Mungu Waefeso 4:12 "Kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe."
Kila mshiriki ana jukumu maalum 1 Wakorintho 12:13, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani ikawa tu watumwa au ukawa tu huru nasi tulinyweshwa Roho mmoja."
Wakristo tu wafariji wenzetu Waebrania 10:25 "Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Hivyo naenda kusema kuwa ndiyo sababu siku zote nikijitazama kama kijana humuona Mungu kuwa ni wa ajabu kuniumba hata mimi na kunifanya kuwa Mchungaji. Hivyo hukubaliana na nyimbo na waimbaji hawa ambao wamewahi sema kupitia nyimbo zao kuwa

a.            “Mungu wetu ndiye Boma”- Tumwabudu Mungu Wetu 302 na Dr. Martin Luther
Mungu ndiye ngao yetu na siraha yetu shetani akija kwetu tukiwa naye daima tutashinda na maadui zetu (shida,adha na changamoto za maisha yetu  yote). Tumtazame yeye kama Dr. Martin Luther alivyosema katika maneno ya wimbo wake huu. Anaimba wakati akiwa katikati ya mapambano na sisi tuimbe tunapopita katika hali mbalimbali katika maisha yetu.



b.            “Mungu ni Mwaminifu”. -Solomon Mkubwa
Mungu hatotuacha daima yeye hutunza maagano(makubaliano yetu nay eye) hivyo hata sisi tulivyo hapa anatujua na anaendelea kutunza uaminifu wake kwetu hivyo na sisi tusimame kwake tu, tumtazame yeye pekee.

c.            “Liseme kwani ni jambo usilolijua”- Sarah K
 kwani ni hakika hatuna tunalolijua katika maisha yetu ni yeye (Yesu) anatuwezesha ,ametuwezesha na ataendelea kutuwezesha.

d.            “I will be There, Just Call My name”. -Michael Jackson&Mariah Carey
Ipo siku tutaitwa kwenda Mbinguni na kila mmoja wetu ataitwa kwa jina lake; hivyo tujiandae.

e.            “Heri Kumjua Yesu Bwana”.  Tumwabudu Mungu Wetu 175 na F.J Crosby
Ni Yesu pekee atatuwezesha na kutuvusha na hata sasa anajua tulikotoka,tulipo na tuendako.

f.             “Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana”. Tumwabudu Mungu Wetu 268 na samuel Stone
Kama tulivyoimba siku ile ya Kipaimara hebu tuendele kumtazama yesu kama msingi wa Kanisa na ndiyo njia pekee ya kutuvusha vijana, njooni tumtumikie kadili ya nafasi tunazojali. Tusiogope huku ni kuzuri tu hakuna shida yoyote.

LEO HII NAKUONA KIJANA MWENZANGU KAMA:-
  1. MSHARIKA MKAMILIFU ALIYEPO NA AJAYE

  1. KIONGOZI WA KANISA-MZEE WA KANISA-MTUMISHI WA MUNGU KADA MBALIMBALI


  1. MLEZI WA FAMILIA   AJAYE NA ALIYEPO (wajibu wako pale nyumbani kwa sasa).

  1. MZAZI AJAYE – (unayoyafanya sasa nawe utafanyiwa na m/watoto wako).
  2. MTETEZI WA WANYONGE (Haki za wanyonge na wanaonyanyaswa kuto kaa kimya kwani Dr. Martin Luther alisema utawajibika kwa yale uliyoyasema na usiyoyasema lakini ulipaswa kuyasema na umekaa kimya.)


  1. MWANA MAENDELEO ( Jiandae kuajili au kuleta mabadiliko katika eneo ambalo Mungu atakupa/amekupa).

A.    “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…” (Mhubiri12:1)

B.    “Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu  linakaa ndani  yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”.
             (I Yohana 2:14b).

C.   Na nimwibie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mzabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu,kilimani penye kuzaa sana;akafanya handaki kulizunguka pande zote, akatwaa mawe yake,akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, akajenga mnara katikati yake, akachimba shinikizo ndani yake;akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, nao ukazaa zabibu-mwitu. Na sasa, enyi wenyeji wa yerusalem, namyi watu wa Yuda amueni, nawasihi mkato, kati ya mimi na shamba  langu la mizabibu….”(Isaya 5:1-7). 


UELEWA JUU YA UJANA NA KIJANA
1.     Ujana ni hatua ambayo mtu anaipitia baada ya utoto au ni kipindi cha kati cha makuzi ya mtu kabla ya utu uzima na hatimae uzee
2.    Ujana huanza mara baada ya mtu kubadilika kimaubile na huanzia miaka kumi na mbili wengine hadi kumi na tano ambapo mtu huanza kuwa na hisia za kimwili na kutamani sana kuwa na uhuru wake katika maamuzi. Mabadiliko haya huchochea au hupelekea hisia mbalimbali za kimwili na mabadiliko ya jumla ya tabia
3.    Ujana ni majira yanayopita katika makuzi ya mwanadu, ukifanikiwa kuwa mzee ni lazima ulipita katika kipindi hiki au daraja hili la ujana, kwa hiyo kama bado uko katika dara hili ni muhimu kujipanga ili usije ukajilaumu mbele ya safari
ZINGATIA HII
“Huwezi kuyajali maisha yako kama hujui thamani yake, huwezi kujua thamani ya maisha yako kama hujajitambua kwa Neno la Mungu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio kama maamuzi yako hayatengenezi mafanikio, ufahamu sahihi juu ya maisha yako ndio msingi wa kujitambua kwako, yaani kuijua Kweli ili hiyo Kweli ikuweke huru na ndipo utakapokuwa huru kweli kweli, kumbuka hata usipoamua maisha yako yataendelea kama kawaida. Zaidi ya hayo kama hujui wewe ni nani huwezi kujua thamani yako, kama hujui thamani yako lazima utaishi chini ya kiwango cha maisha unayotakiwa kuishi”.
UTAIJUAJE NAFASI YAKO KAMA KIJANA
Nafasi yako kama Kijana ni wajibu wako, umuhimu ulionao kwako na kwa jamii kwa ujumla wake pamoja na familia yako. Lazima ujue nafasi yako katika maeneo yafuatayo:
• Kwako binafsi,
• Katika familia yako,
• Kwa Kanisa lako,
• Kwa jamii yako
• kwa mkoa wako,
• kwa Taifa lako na
• kwa Ufalme wa Mungu.
Safari ya kujua nafasi yako katika maeneo yako hayo  hayo hapo juu  inaanzia katika eneo moja tu ambalo ni KUJITAMBUA
KUJITAMBUA NI NINI
“Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata.
HIVYO BASI KIJANA ANATAKIWA  KUJUA KUWA:-
1. Kujitambua ni hatua ya muhimu katika maisha ya mtu yoyote duniani kama anataka kuishi kwa Furaha na matumaini na kufikia malengo yake
2. Kujitambua ni matokeo ya kupata ufahamu sahihi juu eneo fulani utakaokusaidia kufanya maamuzi sahihi katika eneo husika ili uweze kufanikiwa
3. Ufahamu au maarifa unapatikana kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa mbalimbali kwani si kila namna ya kujitambua ni sahihi kwa kijana
4. Matokeo ya ufahamu ulionao yatafanana na ubora wa maisha unayoishi kwa kiwango cha kuathiri maamuzi yako ya kila siku
5. Kiwango cha matokeo ya kujitambua kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata
6. Udhihirisho wa maisha ya kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha kwamba kweli umejitambua.
KUJITAMBUA NI LAZIMA KWANI:-
1. Ni lazima ujitambue, upate ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo yote na jamii inayokuzunguka
2. Ni muhimu ujue wajibu ulionao kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya maisha yako
3. Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu wako kwa wazazi na familia kwa ujumla
4. Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako, Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda lakini usifikiri mafanikio hayako Tanzania
5. Kijana unatakiwa ujitambue, ujielewe  kuwa wewe  ni nani na una kusudi gani katika maisha yako
6. Unatakiwa kupata uelewa wa kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake ukiwa bado Kijana ili ujue namna ya kuzingatia na kujipanga kwa hapo baadae
7. Kuelewa changamoto zilizopo katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda kuna uhusiano na namna unavyojitambua ukiwa bado kijana
8. Kujenga shauku, nia na kiu kwa kijana ili aweze kuishi maisha yenye mwelekeo na aweze kutimiza maono yake akiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yake kwa ujumla wake
9. Kuwekeza uthamani na nguvu ya kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu.
Imeandaliwa na
Mchg Kurwa Sadataley- Mratibu wa Idara
 Habari na Mawasiliano KKKT-DIRA


NI KATIKA TAMASHA LA REDIO FURAHA HIVI SASA
REDIO HII INAMILIKIWA NA K.K.K.T -DAYOSISI YA IRINGA   
INAITWA REDIO FURAHA 96.7 FM PIA UNAWEZA ISIKILIZA KWA MASAFA KUPITIA INTERNET KATIKA BLOG HII INGIA PALIPO ANDIKWA REDIO FURAHA 
SASA NI WAKATI WA CHAKULA