Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, January 28, 2013



            MAHAFALI YA KIDATO CHA  SITA 2012/2013

Zaidi ya wanafunzi 70 wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Pomerini, wilayani Kilolo, mkoani Iringa leo wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya kidato cha sita.

Shule ya sekondari hiyo imefanikiwa kwenye baadhi ya mambo yakiwamo ya kuwa na shamba la miti, kuletea shule tuzo ya medali ya dhahabu kwenye utunzaji wa mazingira. 


         "ASKOFU  MDEGELLA AKIDUMISHA MILA"

    

                         JE NI KILIMO KWANZA AU USAFIRI KWANZA?


VIONGOZI WA DINI NA SAKATA LA GESI

      
                                  Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu
                      Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akizungumza na viongozi wa Dini huko Mtwara
                                                     Katika Ukumbi wa Veta Januari 28,2013

Viongozi wa dini waliojitosa kwenye mgogoro huo ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a na Askofu Mteule wa Kanisa la KKKT, Dayosisi Mpya ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbedule.
Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamepinga mradi wa kusafirisha nishati hiyo kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa hawaoni ni namna gani utawanufaisha wakazi wa Mtwara.
Askofu Mnung’a alisema anapingana na uamuzi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na badala yake kuishauri Serikali ijenge mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara.
“Lazima wananchi wa Mtwara waamke, tumejifunza kule Songosongo, gesi imekwenda Dar es Salaam, si Kilwa wala Lindi iliyofaidika na gesi ile… gesi ibaki Mtwara, mikoa ya kusini iimarishwe,” alisema Askofu Mnung’a na kuongeza:
“Hii yote ni Tanzania, hakuna ubaya wowote ile mitambo ya kufua umeme ikawekwa Mtwara… wafikirie leo hatuombei ila watu wakilipua Kidatu (Morogoro), nchi itakuwa gizani, lazima tutawanye rasilimali zetu siyo kila kitu Dar es Salaam.”
Askofu huyo alimpongeza Murji kwa kuweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo na kumshangaa Mbunge wa Masasi Mariam Kasembe anayeunga mkono akisema, mbunge huyo hawakilishi maoni ya wananchi.
“Nimewaambia waumini wangu kuwa tuwe tayari kutetea rasilimali yetu…. nampongeza Murji kwa kutetea masilahi ya wananchi,” alisema Askofu Mnung’a.
Askofu Mbedule alisema hapingi gesi kwenda Dar es Salaam ila hadi pale ahadi za Serikali zitakapotimizwa kwa wananchi wa Mtwara.
“Kwenye salamu zangu za Krismasi niliwaambia waumini kuwa ni wakati wa kuidai Serikali kutimiza ahadi zake kwa wananchi… wananchi wa Mtwara waliahidiwa viwanda, hakuna kiwanda hata kimoja, gesi inaondoka... hapana sikubaliani nalo,” alisema Mchungaji Mbedule na kuongeza:
“Serikali itueleze bomba la gesi kwenda Dar es Salaam litatoa ajira ngapi kwa wananchi wa Mtwara? Hilo moja, pili bomba hilo litachochea vipi uwekezaji kwa mikoa ya kusini… kama hakuna majibu ya hayo basi mimi nazuia gesi isiende Dar es Salaam.”
Alisema Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi neema wananchi wa Mtwara kutokana na uchimbaji wa gesi na kwamba kabla ya kufikiria kuisafirisha kwenda Dar es Salaam ni muhimu ahadi hiyo ikatekelezwa.
“Zaidi ya miaka 21, Barabara ya Mtwara - Dar es Salaam haijaisha, mikoa mingine zinajengwa barabara zenye kilomita nyingi na zinakamilika na kuiacha hii ya kusini… hata juzi nimepita hapo bado barabara ni ya vumbi,” alisema.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1656316/-/vjlvwc/-/index.html  Jumatano 30 Januari,2013

UBARIKIO WA WACHUNGAJI 2013

NI UBARIKIO WA WACHUNGAJI SABA


                      


  




 
 

 
 
 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 







"SHULE ZETU ZIMEANZA  KUONESHA MWANGA"

MANENO  YA BABA ASKOFU DKT. O.M. MDEGELLA MARA BAADA YA AFISA MAFUNZO KUBANDIKA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2013

MATOKEO HAYO YAMEBANDIKWA KATIKA UBAO WA MATANGAZO KATIKA OFISI ZA DAYOSISI MAARUFU KAMA "DIRA"