Manara awajia juu wanaokejeli ushindi wa Simba, "Mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini"
Writen by
sadataley
3:26 PM
-
0
Comments
Msemaji wa kloabu ya Simba, Haji Manara, amewajia juu watu ambao wanabeza matokeo ya ushindi wa bao 1-0 walioupata usiku wa jana kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.
Katika ushindi huo bao hilo pekee la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya dakika ya pili kipindi cha kwanza. Hata hivyo mashabiki wengi mitandaoni wamekuwa wakiubeza ushindi huo ukionekana ni mdogo sana tofauti na matarajio ya wengi ambapo ukilinganisha na ukubwa wa kikosi cha Simba kwa sasa.
kutokana na maneno hayo Manara kupitioa mtandao wa Instagram ameamuakuwajibu kwa kuandika:
Salaam
wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!!
Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons!!
Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu..hisabati 3×3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane.\
Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!
Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!
Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!
Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!
Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu.
Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha.
Ni lazma mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu.
Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc..na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo..
Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina kasparov na karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu
Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..usifate mkumbo wa mitandaoni
No comments
Post a Comment