Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, September 2, 2017

Ni nini kinachofanyika ubongoni mwa mtu akipiga miayo

Unaweza kuwa unapiga miayo hivi sasa wakati ukisoma taarifa hii - ni wa kuambukiza.
Sasa watafiti wamekuwa wakichunguza kinachofanyika ubongoni ili kuchochea hali hiyo.

Timu ya watafiti katika Chuo kikuu cha Nottingham, imegundua kinachofanyika kwenye sehemu ya mwendo ndani ya ubongo wa binadamu.

Sehemu ya primary motor cortex pia inatumika pakubwa kwenye hali kama Tourette's syndrome, yaani kinachofanyika wakati mtu anapopatwa na ugonjwa wa neva.

Kupiga miayo mara kwa mara, ni dalili ya echophenomena - yaani namna ya kuiga maneno ya mtu mwingine matendo bila ya kujua.

Hali hii ya Echophenomena pia inaonekama katika Tourette's, pia katika hali ya mtu kuugua kifafa na tawahudi.

Ili kufanyia uchunguzi kile kinachofanyika ndani ya ubongo wa mtu wakati wa hali hiyo ya kupiga miayo, wanasayansi waliwachunguza watu 36 waliojitolea, huku wakiwachunguza wengine wakipiga miayio.

'Excitability' ni hali ya kuweza kusisimuliwa kufanya kitu sawa na anachofanya mtu mwingine.

Katika utafiti huo, ambao umechapishwa katika jarida la biolojia la Current Biology, baadhi yao waliambiwa kuwa ni sawa mtu kupiga miayo, ilihali wengine wakiambiwa kuzuia hali hiyo kufanyika au kukandamiza hamu.

Kwa ujumla, hamu ya kupiga miayo iliamuliwa kuwa ni namna kila motor cortex ya kila mtu inavyofanya kazi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment