Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 4, 2017

Kiongozi wa chama cha upinzani Zambia atiwa nguvuni.

Polisi ya Zambia imemkamata kiongozi wa upinzani wa nchini humo, Saviour Chishimba kwa tuhuma ya kumtukana Rais Edgar Lungu, kosa ambalo adhabu yake inawezeka kufikia kifungo cha miaka mitano jela.

Hakainde Hichilema
Hata hivyo polisi ya Zambia haikuweka wazi matusi yaliyotolewa na kiongozi wa chama cha upinzani cha Progressive People (UPP), Saviour Chishimba dhidi ya Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo. Polisi imesema Chishimba alitoa matusi hayo baina ya tarehe 1 na 8 mwezi uliopita wa Julai.
Mivutano ya kisiasa katika nchi ya Zambia ambayo wakati mmoja ilionekana kuwa miongoni mwa nchi zenye demokrasia imara zaidi barani Afrika, imeshadidi zaidi tangu serikali ya nchi hiyo ilipomtia nguvuni kiongozi mkuu wa upinzani, Hakainde Hichilema kwa tuhuma za uhaini mwezi Apili mwka huu.

Tarehe 6 Julai Rais Lungu wa Zambia alisema kuwa, ameruhusu kutumiwa mamlaka ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya uharibifu ambavyo alidai vinavyofanywa na wapinzani wake wa kisiasa baada ya moto kuteketeza soko kubwa katika nchi hiyo ya kusini mwa Afika.
Msemaji wa polisi ya Zambia, Esther Mwaata-Katongo amesema Saviour Chishimba anashikiliwa kizuizini na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.  
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment