Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 3, 2017

ZIDANE ampa ujiko Ronaldo, asema ni mchezaji bora kuliko yeye

KOCHA wa Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane amesema kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko alivyokuwa yeye enzi zake.

Zidane anatumaini Ronaldo ataiongoza Real kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo, itakapomenyana na Juventus ya Italia mjini Cardiff usiku wa Jumamosi.

Ronaldo amefunga jumla ya mabao 49 kwa klabu na nchi yake msimu huu na amefunga hat-tricks (mabao matatu katika mchezo mmoja) kwenye hatua zote, Robo Fainali na Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa.

Alipoulizwa katika mkutano na Waandishi wa Habaru, nani angekuwa bora kama wawili hao wangecheza zama moja, mshambuliaji gwiji wa Ufaransa Zidane, akasema: "Ronaldo, hakuna shaka.

"Anafunga mabao na hilo ndilo muhimu zaidi. Nilikuwa nacheza vizuri mno, lakini kufunga mabao siku mtu maalum. Nilikuwa mzuri katika kutengeneza nafasi za mabaoa. Nilifunga mabao fulani muhimu, lakini si megi kama yeye,'alisema.

Zidane alizichezea zote, Real na Juventus enzi za ujana wake.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment