Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, June 16, 2017

Warepublikan, Wademokrat washikamana baada ya Scalise kupigwa risasi

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakiongea na Dkt. Ira Y. Rabin, baada ya kumtembelea Mbunge Scalise hospitali.

Wabunge wa Marekani wakiwa wamehuzunika wameahidi kushikamana pamoja Alhamisi na kuweka pembeni tofauti zao.
Pande zote mbili-- Warepublikan na Wademokrat --walieleza hayo baada ya kikundi cha Wabunge wa Republikan na wafanyakazi wao kushambuliwa kwa risasi katika mazoezi ya mchezo wa baseball Jumatano.
Habari za kushtusha zinazohusu kiongozi wa ngazi ya juu, katika Chama cha Republikan, Steve Scalise kuwa ni kati ya wale waliojeruhiwa kwa risasi, imeleta malumbano ya kawaida katika mjadala wa kisiasa hapa Washington.
“… Democrats wamesimama pamoja na wenzao Warepublikan wakitafakari mashambulizi yenye kushitusha,” wote kwa pamoja walisikika wakiahidi kuwa na mshikamano.
Spika wa Bunge la Marekani Paul Ryan amesema: “Sisi ni kitu kimoja ndani ya bunge, hili ni bunge la watu, tunaungana katika masuala ya kibinadamu, na ni ubindamu ndio utakaoshinda mwisho wa siku.”
Imeelezwa kuwa siku ilianza Jumatano baada ya Mbunge Scalise kupigwa risasi pamoja na wafanyakazi wawili wa Bunge na maafisa wa polisi wa Kituo cha Capitol… Kuwepo kwa maafisa hao wa polisi kuliepusha janga kubwa, amesema mbunge Joe Barton alipokuwa akiondoka katika uwanja wa michezo ambao uligeuka kuwa ni sehemu ya tokeo la jinai…
Mbunge Joe Barton amesema: “Askari wa Capitol Hill waliokuwepo katika ulinzi wakati wa mazoezi hayo ya baseball waliokoa maisha yetu.”
Warepublikan, waliokuwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wa hisani wa baseball ulioandaliwa na bunge la Marekani.

VOA Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment