Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, June 16, 2017

Mkuu wa Mashtaka ICC atoa wito Saiful-Islam Gaddafi akamatwe

Mkuu wa Mashtaka wa ICC Fatou Bensouda.
Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ametoa wito wa kutiwa nguvuni na kukabidhiwa Saiful-Islam Gaddafi anayetafutwa kwa kuhusika na jinai za kivita kwa kuwakandamiza wapinzani wa utawala wa baba yake, kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi.
Fatou Bensouda ametoa taarifa jana Jumatano akieleza kwamba: "Natoa wito kwa Libya na serikali nyengine zote, ikiwa zitakuwa katika nafasi ya kufanya hivyo, zimkamate mara moja na kumkabidhi bwana Gaddafi kwa ICC". 
Siku ya Jumapili iliyopita, Zaidi, wakili wa Saiful-Islam alitangaza kuwa mteja wake ameachiwa huru kutoka jela ya mji wa Zintan aliokuwa akishikiliwa tangu mwaka 2011, kwa mujibu wa sheria ya msamaha iliyopasishwa na bunge.
Kwa mujibu wa ripoti, Saiful-Islam Gaddafi aliachiwa huru siku ya Ijumaa na aliondoka siku hiyo hiyo katika mji wa Zintan ulioko kaskazini magharibi mwa Libya na kuelekea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa Zaidi, Saiful-Islam Gaddafi anaweza kutoa mchango muhimu katika juhudi za kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba hatojisalimisha kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake The Hague.
Bensouda ameongeza kuwa ofisi yake inajaribu kufuatilia kuachiliwa huru kwa mwana huyo wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya.
Mwaka 2015, mahakama moja ya mjini Tripoli, ilitoa hukumu ya kifo kwa Saiful-Islam Gaddafi mwenye umri wa miaka 44 bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na jinai za vita  ikiwemo kuwaua waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi yaliyohatimisha utawala wa baba yake. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Libya ilitoa taarifa siku ya Jumapili iliyopita na kutangaza kuwa Saif angali anatafutwa kuhusiana na hukumu hiyo ya kifo iliyotolewa dhidi yake.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment