Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 3, 2017

Ronaldo alivyoichakaza Atletico Madrid


Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameendeleza ubabe wake kwa kupiga Hatrick nyingine ya pili mfululizo usiku wa jana kunako dimba la Santiago Bernabeu wakati timu yake ilipovaana na mahasimu wao Atletico Madrid kwenye mchezo wa kwanza hatua ya nusu fainali, Klabu Bingwa barani Ulaya.

Real Madrid-Atletico Madrid 3-0, l'uragano Ronaldo spazza via Simeone
Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake la pili jana usiku dhidi ya Atletico.

Ronaldo alianza makeke yake kunako dakika ya 10′ ya mchezo huo kwa kupiga kichwa kizito kilichopelekea mlinda mlango wa Atletico Madrid kushindwa kuhimili mpira huo na Mreno huyo kucheka na nyavu.

Mpaka mpira unaenda mapumziko Atletico walikuwa wameshatandikwa goli moja,na kipindi cha pili mashambulizi yaliwaelemea zaidi Atletico kwani kunako dakika ya 73,Ronaldo alipiga shuti la mbali lililomuelemea goli kipa kabla ya goli la tatu ambalo alifunga kunako ya 86′ na kumaliza hesabu ya magoli 3-0,Na ikiwa pia ni Hatrick ya pili ya mfululizo baada ya ile aliyowapiga Bayern Munich.

Ronaldo kwa sasa anakuwa ndiyo mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwenye historia ya michuano hiyo tangia ianzishwe akiwa na magoli 104,mbele ya mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi mwenye magoli 98.

Ili Atletico Madrid iweze kutinga fainali ya michuano hiyo itahitaji miujiza ya Mungu kwa Klabu ya Madrid kuruhusu Magoli Manne au zaidi ili ikate tiketi ya kucheza fainali.

Fainali ya Klabu Bingwa barani ulaya itachezwa mnamo tarehe 03/June mwaka huu kunako dimba la Cardiff,huko nchini Uingereza .
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment