Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 16, 2017

Jambazi aliyeuawa na Askari Dar alikuwa akisema "Allahu Akbar, Allahu Akbar"


Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, jambazi aliyeuawa juzi katika eneo la Kurasini, Manispaa ya Temeke, na wenzake wawili kutoroka, alikuwa anataka kupora Sh. milioni 360 kutoka katika gari la kampuni ya G4S lililokuwa likizisambaza kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) za CRDB.

Fedha hizo zilikuwa kwenye gari lenye namba za usajili T155 DCB aina ya Nissan mali ya kampuni ya ulinzi ya G4S huku likisindikizwa na askari wawili wa kikosi cha FFU.

Alisema wakati wahudumu wa G4S wakisambaza fedha, mmoja wa watu waliokuwa katika bodaboda hizo ghafla aliruka na kumvamia askari kwa lengo la kumpora silaha ili kufanikisha zoezi la uporaji wa fedha hizo. Alisema kuwa baada ya kitendo hicho jambazi huyo aliamriwa asimame lakini alikaidi na ndipo alipopigwa risasi iliyomjeruhi mguuni na nyingine tumboni kisha aliishiwa nguvu na kusika akitamka " Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar"
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment