Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 17, 2017

Faida ya kutumia ganda la ndizi mbivu

Wengi wetu tukila ndizi mbivu huwa tunatupa maganda ya ndizi, lakini ukweli ni kwamba maganda ya ndizi yana faida lukuki kama ifutavyo;

1.Husaidia kung'arisha meno.

Unachotakiwa kufanya ni;
Chukua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na kisha sugulia kwenye meno itasaidia kuyafanya meno yako kuwa meupe.

2.Husaidia kuondoa vipele vya mbu na wadudu.

Unachotakiwa kufanya ni;
Tumia ganda la ndizi kwa kusugulia sehemu uliyoumwa na mdudu au mbu ili kuondoa maumivu na wekundu.

3. Huondoa mikunjo usoni ( wrinkles)

Unachotakiwa kufanya ni;
Changanya ute wa yai na nyuzi nyuzi za ndani ya ganda la ndizi kisha paka usoni kwa dakika 20, ili kupoteza mikunjo.

Hizo ni faida chache kati nyingi ya kutumia ganda la ndizi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment