Writen by
sadataley
1:32 PM
-
0
Comments
KATIBU WA SHIRIKISHO LA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI NA VYUO VISIVYO VA
SERIKALI (TAMONGSCO), KANDA YA ARUSHA MAGHARIBI, LEONARD MAO.
SHIRIKISHO la wamiliki wa shule binafsi na vyuo visivyo vya serikali, limeiomba serikali kuwapunguzia kodi wanaodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuwa shule hizo zimekuwa zikitoa huduma kwa Watanzania sawa na huduma zinazotolewa na shule za serikali.
Katibu wa Shirikisho la wamiliki wa shule binafsi na vyuo visivyo va
serikali (Tamongsco), Kanda ya Arusha Magharibi, Leonard Mao, alisema
hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kupokea taarifa za utendaji
wa wanachama kikanda, na kujadili changamoto zinazowakabili za ulipaji
kodi nyingi ambazo wanadaiwa wanachama hao.
Alisema wamiliki hao kwa sasa imefika mahali wanashindwa kuendesha shule hizo kutokana na kudaiwa kodi zaidi ya 15 na TRA, hali hiyo inatokana na TRA kutotoa elimu kwa wanachama hao, kuhusu kodi hizo, hivyo shule hizo kujikuta zinashindwa kulipa kwa wakati.
Alisema ni vema serikali ikapunguza utitiri wa kodi zaidi ya 15, ambazo zinawaumiza wamiliki hao, lakini pia kuwafanya kushindwa kuzilipa ili waweze kubaki na kuendeleza shule hizo.
Naye Katibu wa shirikisho la wamiliki wa shule binafsi mkoani hapa, Malliasy Mollel, alisema moja ya kero kubwa inayowakabili wamiliki wa
shule binafsi, ni udaiwaji wa kodi ambazo hadi sasa wamiliki hawaelewi umuhimu wake, kwa kuwa TRA ingepaswa kutoa elimu kwanza ya ulipaji wa kodi hizo za mfululizo.
"Wengi wa wanachama wetu tunasumbuliwa sana na TRA, ndio mana wengi tunalalamika kwa kuwa sehemu kubwa tunadaiwa kuwa shule hizi zinafanya biashara jambo ambalo si la kweli, bali tunatoa huduma sawa sawa na zile zinazotolewa na serikali," alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa shule binafsi, mmiliki wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Maua, William Kirika, alisema, shule binafsi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto lukuki, ikiwamo ya mlolongo wa kodi, huku ada ya shule ikiwa ni ile ile.
Alisema hivi sasa hali ya maisha imekuwa ngumu, huku kila kitu kikipanda bei huku kodi zikiendelea kuwa nyingi, hivyo waliomba kupunguzwa kwa kodi hizo kwa kuwa zinawaumiza.
Naye mmiliki wa Shule ya Amani, Wilfred Daniel, alisema, kutokana na mlolongo wa kodi, hali hiyo inaleta mkanganyiko kwa shule nyingi na kuomba elimu zaidi ya ulipaji kodi kuendelea kutolewa kwa wamiliki wa shule.
Mtoa elimu na huduma kutoka TRA, Eugenia Mkumbo, alisema hakuna suala jipya katika ulipaji wa kodi hizo, kwa kuwa ni suala lililopitishwa na serikali. Kama mamlaka ya mapato, wataendelea kutoa elimu, kutokana na mswada huo kupitishwa pia na Bunge na kuwa sheria.
SHIRIKISHO la wamiliki wa shule binafsi na vyuo visivyo vya serikali, limeiomba serikali kuwapunguzia kodi wanaodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuwa shule hizo zimekuwa zikitoa huduma kwa Watanzania sawa na huduma zinazotolewa na shule za serikali.
Alisema wamiliki hao kwa sasa imefika mahali wanashindwa kuendesha shule hizo kutokana na kudaiwa kodi zaidi ya 15 na TRA, hali hiyo inatokana na TRA kutotoa elimu kwa wanachama hao, kuhusu kodi hizo, hivyo shule hizo kujikuta zinashindwa kulipa kwa wakati.
Alisema ni vema serikali ikapunguza utitiri wa kodi zaidi ya 15, ambazo zinawaumiza wamiliki hao, lakini pia kuwafanya kushindwa kuzilipa ili waweze kubaki na kuendeleza shule hizo.
Naye Katibu wa shirikisho la wamiliki wa shule binafsi mkoani hapa, Malliasy Mollel, alisema moja ya kero kubwa inayowakabili wamiliki wa
shule binafsi, ni udaiwaji wa kodi ambazo hadi sasa wamiliki hawaelewi umuhimu wake, kwa kuwa TRA ingepaswa kutoa elimu kwanza ya ulipaji wa kodi hizo za mfululizo.
"Wengi wa wanachama wetu tunasumbuliwa sana na TRA, ndio mana wengi tunalalamika kwa kuwa sehemu kubwa tunadaiwa kuwa shule hizi zinafanya biashara jambo ambalo si la kweli, bali tunatoa huduma sawa sawa na zile zinazotolewa na serikali," alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa shule binafsi, mmiliki wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Maua, William Kirika, alisema, shule binafsi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto lukuki, ikiwamo ya mlolongo wa kodi, huku ada ya shule ikiwa ni ile ile.
Alisema hivi sasa hali ya maisha imekuwa ngumu, huku kila kitu kikipanda bei huku kodi zikiendelea kuwa nyingi, hivyo waliomba kupunguzwa kwa kodi hizo kwa kuwa zinawaumiza.
Naye mmiliki wa Shule ya Amani, Wilfred Daniel, alisema, kutokana na mlolongo wa kodi, hali hiyo inaleta mkanganyiko kwa shule nyingi na kuomba elimu zaidi ya ulipaji kodi kuendelea kutolewa kwa wamiliki wa shule.
Mtoa elimu na huduma kutoka TRA, Eugenia Mkumbo, alisema hakuna suala jipya katika ulipaji wa kodi hizo, kwa kuwa ni suala lililopitishwa na serikali. Kama mamlaka ya mapato, wataendelea kutoa elimu, kutokana na mswada huo kupitishwa pia na Bunge na kuwa sheria.
No comments
Post a Comment