Writen by
sadataley
1:35 PM
-
0
Comments
MADEREVA 20 kutoka ndani ya nje ya nchi wanatarajia kuchuana katika
mashindano ya taifa ya mbio za magari yatakayofanyika leo na kesho
mkoani hapa.
Mbatta alisema kuwa mashindano ya magari ni fursa nzuri kufanya biashara, kukuza na kuimarisha sekta ya utalii katika Kanda ya Kusini.
Alisema kuwa kuna njia tano zilizochaguliwa kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yataanzia katika kiwanda cha maji cha Mkwawa kilichopo Iringa Mjini ambao pia ni wadhamini wakuu wa mbio hizo.
"Madereva wa Iringa watakaoshiriki ni pamoja na Ahmed Huwel ambaye anasaidiwa na Maisam Fazal, mimi Mbatta (Msaidizi wangu Sultan Chana) na mwingine aliyeomba kushiriki kupitia timu ya Mkwawa Rally ni Shanto ambaye atakuwa na msaidizi wake ni Rahim," alisema Mbatta.
Aliwataja washiriki wengine wa mbio hizo ni mkongwe Francis Mwakatundu, Gerald Miller wa Arusha na Davis Mosha wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wananchi wa mkoa huo kuchukua tahadhari wakati wa mashindano ya mbio za magari huku akiongeza kuwa mbio hizo zitasaidia kutangaza Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
No comments
Post a Comment