Writen by
sadataley
1:15 PM
-
0
Comments

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika kituo cha kupigia kura katika mji wa Istanbul Aprili 16, 2017.
Kambi inayotetea kura ya ndiyo kuhusu kuongeza mamlaka ya rais chini ya rais Recep Tayyip Erdogan imeshinda Jumapili Aprili 16 katika kura ya maoni, kwa mujibu wa matokeo ya muda ya uchaguzi.
Baada kuhesabu 95% ya kura, Ndiyo ilikua ikiongoza kwa 51.7%, licha ya kwamba Hapana ilikua ikiendelea kushuka. UKwa upande wake, upinzani umesema utaomba zoezi la uhesabuji lirejelewe upya.
Hata kabla ya matokeo rasmi, upinzani umeshtumu kuwepo kwa wizi wa kura na unasubiri kupinga baadhi ya matokeo ya kura, mwandishi wetu katika mji wa Istanbul Alexandre Billette, amearifu. Chama kikuu cha upinzani, CHP, kimengaza pia kuwa mpaka sasa kina matokeo tofauti yaliyotangazwa, matokeo ambayo yanaonyesha kuwa ndiyo ilipata asilimia ndogo ya kura ikilinganishwa na matokeo rasmi yaliyotangazwa.
Chama cha CHP kimesema kuwa kinaweza hata kukataa kutambua matokeo ya 60% ya vituo vya kupigia kura. Sababu ni utata huu baada ya Tume Kuu ya Uchaguzi kutangaza kukubali kusahihisha kura ambazo zilikua bado hazijathibitishwa na muhuri rasmi.
Waturuki milioni 55.3 wametakiwa kupiga kura ya maoni kuhusu kubadili katiba kwa minajili ya kuongeza mamlaka ya rais chini ya rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan Tayyip Erdogan au la.
Itafahamika kwamba vituo vya kupigia kura vilifumguliwa katika mji wa Diyarbakir na miji mingine ya Mashariki mwa Uturuki majira ya saa kumi alfajiri, huku upigaji kura mjini Istanbul , Ankara na miji mingine nchi nzima ukianza majira ya baadaye asubuhi hii.
Endapo Tume Kuu ya Uchaguzi itaidhinisha ushindi huo rais Erdogan atapata mamlaka zaidi kuliko kiongozi yeyote wa Uturuki tangu mwanzilishi wake Mustafa Kemal Ataturk na mrithi wake Ismet Inonu.
No comments
Post a Comment