Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, February 10, 2017

AWAMU YA KWANZA YA WATUMISHI KUHAMIA MAKAO MAKUU YA NCHI – DODOMA TAREHE 10 FEBRUARI, 2017

JHU
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara kuhamia Makao- Makuu ya Nchi, Dodoma inaanza tarehe 10 Februari, 2017.
Miongoni mwa watakao hamia katika awamu hiyo ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ambao ni Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Naibu Makatibu Wakuu wa Nishati na Madini.
Watumishi wengine ni pamoja na Kamishna wa Madini Tanzania, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Maafisa. Jumla ya Watumishi wanaohamia Dodoma Awamu ya Kwanza ni 47.
Aidha, kutokana na uhamisho huo, anuani ya Wizara  Dodoma ni;
Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini,
Barabara ya Kikuyu,
S.L.P 422,
DODOMA
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment