Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 8, 2016

Wahamiaji wazidi kuitesa Uturuki

Umoja wa Ulaya na viongozi wa Uturuki waliokutana mjini Brussels wameshindwa kufikia muafaka wa suluhisho la mgogoro wa wahamiaji. Uturuki inatuhumiwa na Jumuiya ya Ulaya kuwa na wimbi kubwa la wahamiaji wanaovuka ,na kuchukua msaada unaozidi euro bilioni tatu. kutokana na hali hiyo Umoja wa ulaya umeitaka Uturuki kuwachukua wahamiaji ambao hawakukidhi vigezo vya kupata hifadhi na kuongeza jitihada zaidi za kuwazuia kuvuka bahari ya Aegean kuelekea Ugiriki. Raisi wa bunge la Ulaya ,Martin Schulz amesema suala la maombi ya uturuki kutaka kuongezewa euro bilioni tatu ili kulipia huduma za afya na shule kwa ajili ya wakimbizi wanaokaa nje ya kambi bado linajadiliwa katika mkutano huo wa nchi za umoja wa ulaya. Hata hivyo Katibu mkuu wa NATO amesema mkutano huo ulioanza jana unafahamika wazi malengo yake katika nchi ya Uturuki na ukanda wa bahari ulioko upande wa ugiriki. Ameyasema wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,Jens Stoltenberg na Waziri Mkuu wa Uturuki Jens Stoltenberg.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment