Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 20, 2016

Wacuba wajitayarisha kumpokea Obama

Serikali ya Cuba na wananchi wanamsubiri kwa hamu Rais Barack Obama akianza ziara yake ya kihistoria kisiwani humo siku ya Jumapili, akiwa rais wa kwanza wa Marekani kulitembelea taifa hilo jirani katika kipindi cha miaka 90 iliyopita. Wananchi wamegawika kutokana na ziara hiyo, baadhi wakiwa na matumiani kwamba ni tukio la kihstoria kupelekea kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, na kuna wale wanaoamini hakuna kitakacho badilika chini ya utawala wa kikomunisti. Kuna Wacuba kama Yosleny Borroto, anaechukulia ziara hiyo ya kwanza na kiongozi wa Marekani tangu miana ya 1920 ni ishara ya mabadiliko makubwa katika nchi yake. "Amekua moja wapo ya marais wa Marekani wanaotaka kutusaidia.. kutusiadia ili nchi yetu ipate maendeleo." alisema Borroto. Rais Obama anafuatana na baadhi ya wafanyabiashara ikiwa ni ishara ya kuzungumzia masuala ya mikataba mipya ya biashara ingawa vikwazo vya kiuchumi vitaendelea kutekelezwa hadi bunge la Marekani kukubali kuviondowa Lakini wakati huo huo kuna Wacuba wenye wasi wasi kama Oscar Casanella Saint Blancard, anaehisi analengwa na serikali kutokana na urafiki wake na wapinzani. Ana hofu kwamba kuanzishwa kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia kati ya Washington na Havana hautamanisha mabadiliko makubwa bali yake anadhani kutakua na matatizo zaidi. "Suala la kwanza, serikali ya Cuba itakua na tabia gani baada wa ziara, haitotosha kuondowa vikwazo hivyo vya marekani. Kwa sababu kuna vikwazo vya serikali ya Cuba dhidi ya watu wa Cuba, na ninadhani hivyo ndivyo hatari zaidi ." alisema Casanella. Nao wapinzani wakuu wa serikali wamefurahishwa na juhudi za rais Obama. Mpizani Miriam Leiva anasema akiweza kukutana na rais Obama basi atamuambia "nina kushukuru kwa sera zako kuelekea kisiwa chetu ambazo zitaleta afuweni kwa maisha ya Wacuba". Maafisa wa white House wanasema miongoni mwa vipaumbele vya ziara yake ni kukutaka na wanaharakati wanaotetea demokrasia huko Cuba.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment