Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 3, 2016

Mwanafunzi wa Misri kufurushwa US baada ya kumtishia Trump

Mwanafunzi mmoja raia wa Misri anakabiliwa na makosa ya kurudishwa nyumbani kutoka Marekani baada ya kuchapisha katika mtandao wake wa Facebook kwamba yuko tayari kumuua mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump na dunia itamshukuru,kulingana na chombo cha habari cha AP. Emadeldin Elsayed mwenye umri wa miaka 23,hakabiliwi na mashtaka ya uhalifu kufuatia ujumbe huo,lakini alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji mwezi uliopita na atahojiwa ili kubaini iwapo atarudishwa nyumbani Misri. Bwana Elsayed amesema aliandika ujumbe huo kwa sababu alikasirishwa na matamshi ya Trump kuhusu waislamu. Amesema kuwa anajuta kuandika ujumbe huo na kwamba hakulenga kumuumiza mtu yeyote,AP imeongeza.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment