Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 16, 2016

Mwanafunzi Mmarekani afungwa jela Korea Kaskazini

Otto Warmbier alisema alifanya kosa kubwa zaidi maishani mwaka Mahakama ya Juu nchini Korea Kaskazini imemhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Amehukumiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola. Otto Warmbier, 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akiishi na kundi la watalii mjini Pyongyang. Alikamatwa Januari alipokuwa akijaribu kuondoka Korea Kaskazini. Baadaye alijitokeza kwenye runinga akionekana kukiri makosa hayo na kusema kundi moja la kanisa lilikuwa limemuomba abebe kitu cha kukumbuka kutoka kwa safari yake. Korea Kaskazini wakati mwingine huwafunga jela wageni kama njia ya shinikizo kwa mataifa yanayoipinga. Image copyrightfacebook profile Warmbier, 21 alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Virginia. Wakati wa kukamatwa kwake tarehe 2 Januari, shirika la habari la serikali la KCNA lilisema alikuwa ameingia Korea Kaskazini akiwa na lengo la “kuvuruga umoja wa taifa” na kwamba alikuwa amedhibitiwa na kuelekezwa na serikali ya Marekani. Warmbier alipokuwa akikiri makosa Akiongea kwenye runinga Februari, huku akitokewa na machozi, alisema alitenda “kosa kwa kuondoa bango la kisiasa kutoka eneo la kusubiri wafanyakazi katika hoteli ya Yanggakdo”. “Lengo langu lilikuwa kudhuru kujitolea na bidii ya watu wa Korea. Hili lilikuwa lengo la kijinga sana,” alinukuliwa akisema. Alisema ndilo kosa kubwa kabisa alilowahi kulifanya maishani.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment