Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 12, 2016

Mkutano wa Donald Trump wakumbwa na ghasia

Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano. Mkutano huo ulifutwa pia kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wanaohusika na masuala ya usalama wa eneo hilo. Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika nje ya chuo ya Illinois saa chache kabla ya bwana Trump kuwasili. Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri. Ndani ya ukumbi wa mkutano huo vita vilizuka kati ya wafuasi wa na waandamanaji ambao walipeperusha bendera na kutoa matamshi. Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi. Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment