Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, March 11, 2016

Miaka mitano ya kumbukumbu ya janga la Tsunami Japan

Japan imefanya ibada maalumu kuwakumbuka watu 18,000, waliokufa katika tetemeko la Tsunami miaka mitano iliyopita. Katika mji wa Tokyo mfalme Akihito, malkia Michiko na waziri mkuu Shinzo Abe waliongoza maadhimisho hayo Japan Gedenken an Tsunami von 2011 Ilipotimia saa nane na dakika 46, majira ya Japan,watu waliohudhuria kumbukumbu hiyo waliinamisha vichwa vyao pamoja na wakaazi wa maeneo yaliyoathiriwa kutoa heshima na kukumbuka wenzao waliokufa mnamo saa sawa na hiyo tarehe kumi na moja mwezi Machi mwaka 2011, pale tetemeko la Tsunami lenye ukubwa wa 9.0 lilitokea katika bahari Pasific Maji mengi yalibomoa majengo na kusomba vitu na kuathiri vinu vya nyuklia vya Fukushima Daiichi hali iliyosababisha kuvuja kwa mionzi hatari ya nyuklia kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1986. Kwenye hotuba yake mfalme Akihoto alihuzunishwa na wale waliolazimishwa kuhama makwao kutokana na ajali hiyo. "Nahisi Uchungu moyoni nikikumbuka watu ambao bado hawawezi kurejea makwao kwa kuwa maeneo mengine hayawezi kushi watu tena," alisema mfalme Akihito Hali katika eneo la Fukushima ambapo viwanda vya nyuklia viliathirika ingali ya tahadhari. Hali hiyo ilisababisha maelfu ya watu wanaokadiriwa kufikia laki moja kuhama na kuacha nyumba pamoja na mali yao. Japan PK Shinzo Abe Jahrestag Erdbeben Tsunami Fukushima Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe Serikali ya Japan inasema itachukua miongo minne kuondolewa kwa mabaki ya viwanda vya nyuklia vilivyoharibiwa na mengine yakaingia baharini kutachukua zaidi ya miongo minne. Mnamo Jumanne mahakama ya Japan iliamuru kampuni ya nishati Kansai kusitisha kwa muda viwanda vyake vipya vya nishati kwa misingi ya usalama, hali inayo Hata hivyo waziri mkuu Shinzo Abe amekariri haja ya Japan kuzalisha nishati kwa njia ya nyuklia akisema mikakati ya kuunda upya viwanda zaidi itaharakishwa ''Taifa letu lisilo na utajiri wa raslimali haliwezi kufanikiwa bila nishati ya nyuklia ambayo inaleta utengamano wa nishati, na kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na suala la mabadiliko ya tabia-nchi,'' alisema Waziri Mkuu Shinzo Abe Ahadi ya serikali ya Japan imefanya Wajapani kuwa na shaka, kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia. Chanzo:DW SWAHILI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment