Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 24, 2016

Mchina akiri kuiba siri za Marekani

Miongoni mwa siri nyingine, Su na wenzake walisaka siri kuhusu ndege aina ya F-22 Mwanamume mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani. Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha. Wizara ya haki ya Marekani imesema kupitia taarifa kwamba Bw Su alilenga kufaidi kifedha. Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa akifanya kazi nchini Canada mwaka 2014. Alidaiwa kuwa na kampuni ya Kichina ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege iliyokuwa na afisi Canada na alikamatwa akijaribu kupata uraia wa Canada. Alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege zake. Sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela na faini ya $250,000 (£170,000).
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment