Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 14, 2016

Magufuli awateua wakuu 13 wapya wa mikoa

Rais wa Tanzania amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais. Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam. Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo; Afisa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Dar es Salaam Ezekiel Elias Kyunga Geita Salum Mustafa Kijuu Kagera Raphael Muhuga Katavi Emmanuel Maganga Kigoma Godfrey Zambi Lindi Dkt. Steven Kebwe Morogoro Zerote Steven Rukwa Anna Malecela Kilango Shinyanga Methew Mtigumwe Singida Antony Mataka Simiyu Aggrey Mwanri Tabora Martine Shigela Tanga Jordan Mungire Rugimbana Dodoma Said Meck Sadick Kilimanjaro Magesa Mulongo Mara Amos Gabriel Makalla Mbeya John Vianey Mongella Mwanza Daudi Felix Ntibenda Arusha Amina Juma Masenza Iringa Joel Nkaya Bendera Manyara Halima Omary Dendegu Mtwara Dkt. Rehema Nchimbi Njombe Evarist Ndikilo Pwani Said Thabit Mwambungu Ruvuma Chiku Galawa Songwe (Mkoa mpya)
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment