Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 9, 2016

Jua lanaswa na mwezi Indonesia

Watu wamelitaja tukio hilo la miujiza Raia Indonesia wameshuhudia jua likizibwa kikamilifu na mwezi. Indonesia ndio nchi pekee iliyoshuhudia tukio hilo kote duniani. Mamia ya watu walimiminika kushuhudia jua likinaswa na mwezi Hoteli zilizopo katika maeneo mazuri ya kushuhudiwa jua likinaswa zilijaa miezi kadhaa iliopita na katika baadhi ya maeneo ilibidi maafisa watafute nafasi za ziada kwa watalii waliokuwa kwenye maboti. Katika kisiwa cha Belitung mamia ya wageni na watalii wa nchni walikusanyika katika fukwe za bahari kabla ya alfajiri. Wakati jua lilipoanza kunaswa na mwezi walishangilia na baadaye kunyamaza kimya kwa mshangao. Wengi wamelielezea tukio hilo kama 'tukio la miujiza'. Kwa wengi Indonesia, tukio hilo linashirikishwa sana na dini na watu huomba, sherehe za kitamaduni na ngoma zimeandaliwa katika sehemu kubwa la eneo hilo. Wanasayansi pia wamkuwepo hususan katika eneo la Maba katika visiwa vya Maluku ambako tukio hilo limeshuhudiwa kwa dakika tatu, ambao ni muda mrefu kuwahi kushuhudiwa jua likinaswa na mwezi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment