Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 7, 2016

Bomu la laptop lalipuka Somalia

Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia. 2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia. Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop). Mtu aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje ya Mogadishu,kundi la kiislamu la Al- Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria. Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al-Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria. Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi (laptop). ''Afisa wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2 yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa (printer).Chanzo:BBC SWAHILI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment