Writen by
sadataley
5:46 PM
-
0
Comments
Sakata la Escrow baadhi mahakamani

Wakati serikali ya Tanzania imeanza kuwafikisha mahakamani baadhi ya maafisa wanaotuhumiwa kuhusika na gawio la fedha kutoka akaunti ya Tegeta ESCROW, Chama tawala nchini humo CCM, kimetoa kauli ya kuwachukulia hatua, makada wake wanaohusishwa na kashfa hiyo.
Baadhi ya maafisa wa serikali ambao wamefikishwa jana mahakamani kwa tuhuma za kuingiziwa mamilioni ya fedha hizo katika akaunti zao ni Mkurugenzi Huduma za sheria katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Rugonzibwa Mujunangoma pamoja na Mhandisi Mfawidhi wa Wakala wa Umeme Vijijini Theophilo Bwakea.
Chanzo: BBC
No comments
Post a Comment