Writen by
sadataley
5:12 PM
-
0
Comments
Purukushani bungeni nchini Kenya

Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.

Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Chanzo:BBC
No comments
Post a Comment