Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, November 20, 2014

Yaliyojiri katika maziko ya Askofu Cliopa. Ibada na maziko yaongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Malasusa,maziko yafanyika katka eneo maalum lililolotengwa katika viwanja vya Kanisa Kuu Njombe.



Waombolezaji wakiwa katika mazishi

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Katikati, akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mh. Filip Mangula katika mazishi ya Askofu mstaafu






Mjane wa marehemu

Mama mjane wa marehemu akiweka Udongo katika Nyumba ya Milele ya askofu Cliopa






 

 
Mkuu wa Kanisa KKKT akiweka shahada la maua katika Kaburi 
 

Mama njane akiweka taji la maua




Shehe wa Mkoa wa Njombe akiweka taji nae.


Mkuu wa mkoa alipata nafasi ya kutoa neno la faraja kwa wafiwa

Kiongozi wa mkuu wa KKKT Tanzania, Malasusa akizungumza na mamia ya waombilezaji 

 

KIONGOZI Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kiluteri (KKKT) Alex Malasula amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali hapa nchini kuacha mara moja kufanya uovu wa kutumia vibaya mali za Umma na kujitete.

Akihubiri katika madhishi ya Askofu Mstaafu wa kanisha hilo jimbo la Njombe, Askofu Cliopa Lukilo, jana aliye fariki Novemba 13, aliwaambia waombolezaji kuw aviongozi wa sasa wamekuwa wakifanya uovu na kujikinga kwa kujitetea kwa wepesi.

Alisema kuwa viongozi wa miaka ya sasa wamekuwa wakifanya maovu ya kutumia vibaya pesa za umma na kuwa wepesi wa kujitetea kwa kucheleweza kudaiwa wakati wakitafuta namna ya kukepa tuhuma.

Alisema kuwa kufanya hivyo si vizuri na kuwasii viongozi kufanya kazi bila kuharibu mali za wananchi kwa kuzitumia vizuri.

Alisema kuwa viongozi wengi hawapendi kutubu na wamekuwa mafundi wa kujitetea kwa kusingizia katiba na kuwa wanasema jambi lipo mahakamani halijadiliki.

“Watu wengi sasa hivi ukiwaambia kutubu hawakuelewe wanatishia watu kuwashitaki, wansema jambo hili lipo mahakamani halijadiliki, mara umenichafua, dawa ya zambi ni kutubu na sio kujitetea,” alisema Malasula.
Alisema ukiona kitu kinacheleweshwa cheleweshwa ujue kinatafutiuwa namna ya kujitetea.
  
Malasusa alisema kuwa Marehemu alikuwa akipigania haki za watoto wakike kwa kufungua shule ili kuwaondoa katika kazi za ndani.

Alisema kuwa ni vyema wanadam wakatambua wakati wowote wanaweza kuitwa kwani marehemu aliwahi kuugua lakini sasa amefariki bila kuugua .

Alisema kuwa marehemu alifariki siku nne baadae baada ya kusema kuwa yeye amejiandaa kufa wakati akifungua mkutano wa umoja wa wanawake wa makanisa mkoani Njombe.

Alisema kuwa marehemu alitaja mara nne kuwa amejiandaa kwa akisema “Mimi nimejiandaa kufa, mini nimejiandaa kufa vizuru” alisema wakati wa kufungua mkutano huo na kufa siku nne baadae.

Aidha kanisani hapo zilizomwa salamu za rambilambi kutoka katika viongozi mbalimbali kutika hapa nchini na nje ya nchi huku kwa hapa nchini Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa salamu zake zilisomwa kanisani hapo.

Viongozi wa serikali katika mazishi hayo alihuzuria mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi, ambapo aliomba viongozi wa dini kuwaombea viongozi wa Umma ili kuepuka na maovu.
 
Dr. Nchimbi alisema kuwa viongozi waombewe ili wasiweze kutafuna mali za umma na kuwa watiifu wanavyo ongoza wananchi mpaka wanamaliza mda wao wa kuongoza kwani viongozi hao ni moja ya kondoo wanao wachunga. 
Habari na http://eliabu.blogspot.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment