Writen by
sadataley
10:03 AM
-
0
Comments
Na Ibrahim Yamola, MwananchiDar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2014 ambayo yanaonyesha kupanda kwa kiasi kikubwa cha ufaulu kutoka asilimia 87.85 mwaka 2013 na hadi 95.98 mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Necta,
orodha ya kumi bora imetawaliwa na shule nyingi zenye majina yasiyo
maarufu, huku shule maarufu ya sekondari ya Tambaza na ya Ufundi ya
Iyunga zikiwa miongoni mwa shule 10 zilizoshika mkia.
Hata hivyo, ufaulu wa mwaka huu unaonekana
kuchangiwa na idadi ndogo ya watahiniwa kulinganisha na mwaka jana, hali
ambayo imejionyesha pia kwenye idadi ya wanafunzi waliohusika na
udanganyifu ambao mwaka huu ni wawili tofauti na wanne wa mwaka jana.
“Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kutumia
fursa hii kuzipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Wilaya,
wakuu wa shule na wasimamizi wa mtihani uliofanyika Mei, 2014 kwa
kuzingatia na kusimamia taratibu za uendeshaji mitihani na hivyo kuzuia
udanganyifu kufanyika,” alisema kaimu katibu mtendaji wa Necta, Dk
Charles E. Msonde wakati alipozungumza na waandishi wa habari jana.
“Aidha Baraza linawapongeza watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2014 kwa kutojihusisha na
udanganyifu,” aliongeza katibu huyo ambaye alijikita katika taarifa
aliyoiandaa kutangaza matokeo hayo.
Mwaka huu waliofanya mtihani walikuwa 40,695 na
waliofaulu ni 38,905 ambao ni sawa na asilimia 95.98, wakati mwaka 2013
watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 50,611 na waliofaulu walikuwa
44,366 sawa na asilimia 87.85.
Katika matokeo hayo, wavulana wameendelea kufanya
vizuri katika masomo ya sayansi huku wasichana wakifanya vyema katika
masomo ya lugha na biashara.
Dk Msonde alisema ufaulu wa mitihani umeimarika ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Watahiniwa wa shule, kati ya 35,650 waliosajiliwa
ni 35,418, sawa na asilimia 99.35, walifanya mtihani. Wasichana walikuwa
11,022 sawa na asilimia 99.63 na wavulana walikuwa 24,396, sawa na
asilimia 99.22.
Dk Msonde alisema watahiniwa wa kujitegemea
waliosajiliwa walikuwa 6,318. Kati yao, watahiniwa 5,277 (asilimia
83.52) walifanya mtihani na watahiniwa 1,041 (asilimia 16.48)
hawakufanya mtihani.
“Jumla ya wasichana waliofaulu ni 12,080 sawa na
asilimia 97.66 wakati wavulana ni 26,825 sawa na asilimia 95.25 ya
watahiniwa wote 38,905 waliofanya mtihani,” alisema Dk Msonde.
“Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata
watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na
asilimia 85.73 wamefaulu katika madaraja I-III wakiwamo wasichana 9,954
sawa na asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia 83.53.”
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Matokeo-kidato-cha-sita-yatia-fora/-/1597296/2386998/-/11hwq0oz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Matokeo-kidato-cha-sita-yatia-fora/-/1597296/2386998/-/11hwq0oz/-/index.html
No comments
Post a Comment