Writen by
sadataley
11:14 AM
-
0
Comments
Rais Obama katika mojawapo ya mikutyano na waandishi wa habari White House, Washington D.C Agosti 9 2013. ©Jason Reed/Reuters |
Ikiwa ni takriban zaidi ya watu 70,000 wakiwa wamesign waraka (petition) wakitaka Marekani kutoa msaada kwa Misrii kwa masharti kwamba wakristo walindwe dhidi ya fujo zinazoendelea nchini humo, utawala wa rais Obama umeingia matatani mara baada ya kuleta mizaha kwenye suala la amani nchini Misri.
Katika mkutano wa waandishi wa habari, naibu katibu wa habaru wa White House, Josh Earnest alijibu swali kwa utani, jamo lililopelekea umati wa waandishi kutulia kimya katika hali ya kutoamini kama angeweza kuzungumza hivyo ilhali wananchi Misri wanateseka.
"Watu wanauwawa, hasahasa Wakristo wakiwindwa, makanisa yanateketezwa, ni nini hatua ya tahadhari ya Rais nchini Misri?" Liliulizwa swali miongoni mwa wanahabari waliokuwepo. (The President's red line in Egypt)
Lakini jibu la kwanza lilikuwa, "sijabeba kalamu yangu nyekundu leo" (I didn't bring my red pen with me today), jambo ambalo liliwatatiza wanahabari.
Kituo cha haki na sheria cha nchini Marekani kinasema kuwa hakuna aliyecheka wala kutabasamu kuhusu jibu hilo, na kwamba walilaumu utawala wa Obama kwa kufanya utani wakati maisha ya watu yakiwa hatarini nchini Misri, mateso wanayopata wakristo nchini humo sio ya kuchukulia kama utani.
Kumekuwa na ripoti kadhaa za makanisa kuchomwa moto, shule za kikristo, pamoja na wakristo kuuwawa na waislamu ambao wanadai wakristo wamehusika katika maandamano yaliyopelekea Rais Mohamed Morsi kuondolewa madarakani.
Chanzo: Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment