Writen by
sadataley
2:02 PM
-
0
Comments
ZAIDI YA SHILINGI MILIONI KUMI NA SITA ZACHANGWA
Fedha hizo zimechangwa katika harambee iliyofanyika katika Usharika wa Iringa Mjini KKKT Dayosisi ya Iringa siku ya jana 30-06-2013 lengo likiwa ni kumalizia upauaji wa Kanisa la Wilolesi.
Akitoa taarifa ya ujenzi na gharama zinazotakiwa Kasisi wa Kanisa Kuu Mchungaji Huruma Bimbiga alisema kuwa ili kukamilisha zoezi la upauaji jumla ya shilingi milioni kumi(10) zinatakiwa hii ni katika kukidhi mahitaji yote ikiwemo gharama za mafundi.
Baada ya taarifa hiyo washarika na waalikwa walisisimka na kuanza mara moja kuchangia kazi iliyokuwa rahisi sana kwa muendeshaji wa harambee ambaye alikuwa ni Mwenyeki wa Chama cha Mapinduzi Madam Jeska Msambatavangu ambapo zaidi ya shilingi milioni kumi na sita zilichangwa ili kukamilisha upauaji wa Kanisa hilo.
Akitoa shukrani baada ya harambee hiyo Msaidizi wa Askofu Mchungaji Blastone Gavile aliwashukuru washarika wote kwa kusema ni hakika wengi tumejiwekea hazina mbinguni, kwani tulilenga kupata milioni kumi lakini tumepata zaidi hivyo ninawaomba tuendelee kutoa tena na tena ili tukamilishe kazi hii iliyopo mbele yetu.
Na mwisho Msaidizi wa Askofu aliwaomba washarika na watu mbalimbali wenye mapenzi mema na kazi ya Mungu waungane na Usharika wa Kanisa Kuu ili kukamilisha kazi hiyo kwa kuchangia.
Kasisi wa Kanisa Kuu Mchungaji Huruma Bimbiga
Hii ni sehemu ya Kanisa iliyobaki kupauliwa
Muonekano wa Kanisa kwa upande wa mbele
Unaweza changia kupitia Mpesa 0756288322
No comments
Post a Comment