Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, February 14, 2020

Maziko ya Daniel arap Moi: Maelfu ya raia wamiminika Kabarak kumuaga rais mstaafu Daniel Moi

Moi azikwa

Image captionDaniel arap Moi azikwa
Rais wa awamu ya pili wa Kenya hayati Daniel arap Moi amezikwa hii leo baada ya jeshi kutoa heshima kwa kupigiwa mizinga 19.
Maafisa wa kijeshi walitoa heshima kwa kufyatua mizinga lilipo kaburi eneo la Kabarak. Ndege za kijeshi ziliruka kutoa heshima kwa hayati Moi.
Tofauti na mtangulizi wake Mzee Kenyatta, ambaye alipata heshima ya mizinga 21, Mzee Moi alipigiwa heshima ya mizinga 19 kwa kuwa alifariki akiwa tayari ameondoka madarakani.
Mizinga ilifyatuliwa kwa mpangilio wa kila dakika tatu.
Moi amezikwa kijijini kwake kaaribu na kaburi la marehemu mkewe Lena aliyeaga dunia mwaka 2004.
Mwili wa rais mstaafu Daniel Moi uliondoka katika chumba cha kuhifadhi mili cha Lee Funeral jijini Nairobi mwendo wa saa moja asubuhi huku msafara wake ukielekea katika uwanja wa ndege wa Wilson ambapo uliwasili nyumbani kwake huko Kabarak muda wa saa mbili na dakika 40.
Mwili huo uliosafirishwa kwa kutumia ndege ya kijeshi uliwasili na kufinikwa na bendera ya Kenya. Ulisindikizwa na msafara wa magari ya polisi , maafisa wa jeshi na familia ya Mzee Moi.
Milolongo mirefu ilioshuhudiwa nje ya chuo kikuu cha Kabarak
Image captionMilolongo mirefu ilioshuhudiwa nje ya chuo kikuu cha Kabarak

Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenya kwa upande wake alisema kwamba anampatia kwaheri mtu aliyemtaja kama babake.
Uhuru anasema kwamba Moi alimlea hadi alivyo sasa akisema kwamba alikuwa mwalimu wake na mshauri wake mkuu maisha yake yote. Amesema kwamba lijifunza siasa kutoka kwa mzee Moi .
Alisema kwamba Kiongozi huyo alikuwa mkali na wakati mmoja alilazimika kujificha kwa muda baada ya kumtaka kukutana naye.
''Nakumbuka nilipopigiwa simu ya kwanza nikamwambia mke wangu ashike , ya pili ilipopigwa make wangu akakataa kushika kwa sababu alijuwa moto uliokuwepo. Nilishika simu nikasomewa na nikaambiwa nifike kabarak katika kipindi cha saa moja. Nilijua kile ambacho kilikuwa kinanisubiri hivyobasi niliamua kujificha. lakini baadaye niliomba msamaha na akanisamehe''. alisema rais Uhuru Kenya.
Aliwataka Wakenya kuiga maisha ya mzee Moi katika kila walichokuwa wakikifanya kila siku.

William Ruto

Naibu wa rais William Ruto alisema kwamba licha ya kwamba Moi hakuwazaa yeye na viongozi wengine waliofanikiwa pakubwa kutokana na ulezi wa kisiasa wa rais mstaafu Moi, anamshkuru kiongozi huyo kwa manufaa ya uongozi aliowaletea Wakenya.
Alisema kwamba Moi alipenda sana elimu hivyobasi akatoa elimu kwa Wakenya wote bila ubaguzi.
Maafisa wa Polisi wakiweka usalama
''Tunajivunia wasomi katika mataifa mengi ya kigeni wanaotuletea fedha za kigeni kutokana na elimu bora iliotolewa na Moi wakayti wa uongozi wake'',alisema Kiongozi huyo.
Alimsifu rais huyo mstaafu kwa kwa kuleta amani Afrika na duniani kwa jumla kupitia kupelekwa walinda amani katika mataifa mbalimbali.
Alisema Moi alikuwa na chama thabiti kilichomsaidia kuunganisha makabila tofauti ili kuleta umoja nchini Kenya.

Raila Odinga

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga amesema kwamba Moi alikuwa mti mkuu uliowaacha wengi wakiyumba baada ya kifo chake
Amsema ni kutokana na hilo kwamba Wakenya wanafaa kusherehekea maisha yake.
Kiongozi huyo amesema kwamba Moi alikuwa twiga ambaye alikuwa anaweza kuona mbali katika maisha.
Aliongezea kwamba watoto wa viongozi waliokuwepo wana haki ya kupigania wadhfa wowote kama Wakenya wengine wowote.
Jenerali Sumbueiyo{ Aliyekuwa mpatanishi wa amani mazungumzo ya Sudan}
Alisema kwamba Mzee Moi alikuza elimu ya watoto wa kike lakini pia hakusahau mtoto wa kiume.
Anasema kwamba mzee Moi alipendwa kwa mapenzi yake ya kuleta amani katika eneo la afrika.
Sally Kosgei {Aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi wa umma na waziri wa maswala ya kigeni}
Alisema ni kati ya viongozi wachache waliohudumu kipindi kirefu katika serikali ya Mzee Moi.
Anasema kwaba walijadiliana na Moi kuhusu maswala mengi ya kijasusi kuelewana na kutofautiana na mzee Moi.
Anasema kwamba licha ya hayo alilazimika kutotoa siri yoyote.
Anasema kwamba Moi aliwaonya wafanyakazi wa serikali kutojiingiza katika maswala ya kisiasa mabli na kuzozana na wanasiasa.
Francis Ole Kaparo { Aliyekuwa Spika wa bunge }
Alisema kwamba mzee Moi alifanya mambo mengi yasioweza kufanywa kwa muda mrefu.
Anasema kwamba Moi alimuamini na kumpatia wadhfa wa Spika wa bunge baada ya kumwambia ukweli kuhusu kubadilisha kifungu cha 2A ili kuleta siasa ya vyama vingi.
Katika hotuba yake Askofu Silas Yego alisema kwamba mzee Moi alijua kwamba kuna kifo na tayari alikuwa amejitayarisha.
''Wakati mmoja wakati tulipokuwa tunamzika mkewe alisema: Tutazika mama hapa na mimi hapa''.
Askofu huyo alisema kwamba Moi wakati mmoja Moi alimuita na kumwambia kwamba andhani safari yake ya kwenda mbinguni imeanza hivyobasi akasema nimuombee.
Askofu huyo anasema kwamba rais huyo mstaafu alitaka watu kumuamini Yesu alipendelea kusoma biblia na kupenda maisha ya kusamehe.
Kiongozi huyo wa kidini aliwaomba wanasiasa kuleta umoja miongoni mwa raia badala ya kujenga uhasama.
Helikopta ya kijeshi iliobeba mwili wa rais mstaafu Daniel Moi
Katika kaunti ya Nakuru ambayo ndio kaunti ya nyumbani kwa Moi waombolezaji walikaidi baridi ya asubuhi kutafuta maeneo watakayotazama mazishi hayo kwa kuweka milolongo mirefu katika uwanja wa chuo kikuu cha Kabarak siku ya Jumatano.
Maziko ya Daniel Arap Moi: Je ni vipi wazee wa jamii huzikwa katika jamii ya Tugen?
Maafisa wa usalama walionekana katika lango la chuo hicho mapema na walikuwa wakiwakagua waombeolezaji.
Raia walianza kuwasili katika uwanja huo mwendo wa saa kumi alfajiri . Baada ya kufanyiwa ukaguzi mkali wa kiusalama waombolezaji walipewa mkate na soda kabla ya kuingia.
Ukumbi wa ibada ya mwisho kabla ya kufanyika kwa maziko ya Moi
Miongoni mwa umati wa watu uliohudhuria mazishi hayo
Kufikia mwendo was saa moja asubuhi , maelfu ya waombolezaji walikuwa wamemiminika katika uwanja wa chuo kikuu cha kabarak.
Waliohudhuria mazishi hayo walikabidhiwa mikate na soda kila mmoja
Image captionWaliohudhuria mazishi hayo walikabidhiwa mikate na soda kila mmoja
Tayari ibada ya mwisho imeanza. Moi atazikwa nyumbani kwake huko Kabarak baadaye hii leo katika maziko ya kitaifa ambayo yanafanywa na jeshi.
Raia wakipanga milolongo mirefu ya kuingia katika chuo kikuu cha Kabarak ambapo mazishi ya danile Moi yanatarajiwa kufanywa
Image captionRaia wakipanga milolongo mirefu ya kuingia katika chuo kikuu cha Kabarak ambapo mazishi ya danile Moi yanatarajiwa kufanywa

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment