Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 24, 2018

Human Rights Watch: Satalaiti zinaonyesha kuwa jeshi la Myanmar linaendeleza jinai


Utawala khabithi wa Kizayuni unahusika katika kulisaidia jeshi la Myanmar kutekeleza mauaji dhidi ya Waislamu
Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa picha zilizochukuliwa kwa njia ya satalaiti zinaonyesha kwamba jeshi la Myanmar na magaidi wa Kibudha wa nchi hiyo, wanaendelea kuharibu na kuyachoma moto makazi ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini humo.

Jeshi la Myanmar likiendelea kuwafuatilia Waislamu wa Rohingya wasio na ulinzi ili kuwaua
Ripoti iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, picha za satalaiti ambazo zilichukuliwa hivi karibuni na Human Rights Watch na kuchunguzwa, zinaonyesha kwamba tangu tarehe tisa hadi 13 mwezi huu, kwa akali vijiji viwili vya Waislamu wa Rohingya kaskazini mwa jimbo la Rakhine, vimeharibiwa kikamilifu na kwamba hujuma hizo bado zinaendelea.
Kufuatia hali hiyo shirika hilo limelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la umoja huo kufanya haraka kuingilia kati kadhia hiyo na kuzuia mwenendo huo wa uharibifu wa makazi ya Waislamu hao. Kwa mujibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch, tangu mwishoni mwa mwaka jana 2017 kwa akali vijiji 55 kaskazini mwa jimbo hilo vimeharibiwa kabisa. Katika uwanja huo, Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema kuwa nyaraka zinaonyesha kwamba, hadi sasa hali ya Waislamu wa Rakhine nchini Myanmar ni mbaya sana na kwamba kila siku makumi ya Waislamu hao huwa wanawasili katika maeneo ya mpakani ya Bangladesh kwa ajili ya kuokoa maisha yao.
Licha ya Umoja wa Mataifa kulitaja jeshi la Myanmar kuwa linahusika na mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu, lakini hadi sasa umoja huo haujachukua hatua yoyote ya maana kwa ajili ya kukomesha jinai hizo za kinyama. Jinai na mauaji makubwa ya jeshi na Mabudha wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa huo wa Rakhine zilianza tarehe 25 Agosti mwaka jana 2017 ambapo katika hujuma hizo maelfu ya Waislamu hao wameuawa na malaki ya wengine kuwa wakimbizi nje ya nchi hiyo.
Parstoday

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment