Writen by
sadataley
3:06 PM
-
0
Comments
Rais mpya wa Afrika Kusini ameahidi kwamba atatwaa mashamba ya kilimo yanayomilikiwa na wazungu nchini humo tangu mwaka 1600 na kuyagawa kwa wazalendo wa nchi hiyo.
Cyril Ramaphosa ambaye aliapishwa wiki iliyopita kuongoza Afrika Kusini baada ya kujiuzulu Jacob Zuma, amesema kutwaliwa mashamba ya wazangu bila ya kulipa fidia ni miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa na serikali yake kwa ajili ya kuharakisha mchakato wa kuwarejeshea umiliki wa ardhi wazalendo wa nchi hiyo.
Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa, mashamba hayo yatachukuliwa kwa njia zinazofaa na bila ya kutumia mabavu na kuongeza kuwa, hatua hiyo haitakuwa na madhara kwa uchumi na sekta ya kilimo ya nchi hiyo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, tangu Afrika Kusini ilipopata uhuru na kufutwa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo (apartheid) katika muongo wa 1990, chama tawala cha ANC kimekuwa chini ya mashinikizo makubwa kwa ajili ya kuondoa dhulma za kimbari na kukomesha udhibiti wa wazungu waliowachache hususan katika sekta ya mashamba na umiliki wa ardhi.
Wazalendo wa Afrika Kusini wanaounda asilimia 79 ya nchi hiyo wanamiliki asilimia 1.2 tu ya ardhi za kilimo nchini humo.
Parstoday

No comments
Post a Comment