Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 24, 2018

Umoja wa Ulaya waitaka serikali ya Tanzania ifanye uchunguzi kuhusu matukio ya mauaji na utekaji nchini

Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko kuhusiana na matukio ya utekaji nyara na mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Tanzania na umeitaka serikali ya Dar es Salaam kufanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo.
Tundu Lissu, mbunge wa Chadema Singida mashariki nchini Tanzania ambaye alinusurika kifo
Taarifa hiyo ilitolewa Ijumaa ya jana kwa ushirikiano wa mabalozi wa nchi wanachama wa umoja huo wanaowakilisha nchi zao ndani ya Tanzania na kuungwa mkono pia na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Canada na Uswisi nchini humo. Taarifa hiyo ilisema, “Tunashuhudia wasiwasi juu ya mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia udhibiti wa kidemokrasia na haki za Watanzania, ndani ya nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa kuwa na utulivu, amani na uhuru.” Mwisho wa kunukuu.
Mwanafunzi Akwilina Akwiline wa chuo cha NIT, aliyeuawa kwa risasi hivi karibuni 
Kadhalika taarifa ya Umoja huo, imesema inasikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita Akwilina Akwilini na kuunga mkono mwito wa Rais John Magufuli wa kufanyikka uchunguzi wa haraka na wa kina kwa ajili ya kuwabaini wahusika wa jinai hiyo. Kadhalika imetaka kuchunguzwa matukio ya mauaji dhidi ya wanasiasa na vitendo vya utekaji nyara watu ambavyo vimeshika kasi hivi sasa ndani ya taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Tunatoa pole za dhati kwa familia zao wahanga wote. Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni nchini, kama vile jaribio lililohatarisha maisha ya mbunge Tundu Lissu, kupotea kwa watu kama mwandishi wa habari Azory Gwanda na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wengine wa kisiasa." Ilisema taarifa hiyo ya Umoja wa Ulaya. Hivi karibuni pia makundi ya kiraia nchini Tanzania AZAKI yalitoa wito wa kuundwa tume huru ya kuchunguza vifo ambavyo vimekuwa vikitokea nchini humo katika mazingira ya kutatanisha hasa katika siku za hivi karibuni.
Parstoday

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment