Writen by
sadataley
10:24 PM
-
0
Comments
Mkutano wa Kimataifa wa kulisaidia eneo la Sahel barani Afrika umefanyika huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji ukihudhuriwa na wakuu wa zaidi ya nchi 30 za Ulaya na Kiafrika kwa kusomwa ujumbe wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Katika ujumbe wake huo wa video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaja mkutano huo kuwa ni hatua iliyochukuliwa kwa wakati kwa ajili ya kudhihirisha azma ya jamii ya kimataifa ya kuziunga mkono serikali na wakazi wa eneo la Sahel barani Afrika ili kuzuia misimamo ya kufurutu ada, kupambana na ugaidi na uhalifu wa kupangwa.
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Kikosi cha askari jeshi cha nchi wanachama wa eneo la Sahel barani Afrika (G-5)
Mogherini pia amesisitiza katika mkutano huo kuwa Umoja wa Ulaya unakiunga mkono kikosi cha wanajeshi wa nchi watano wanachama wa kundi la G-5.

Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani
Mkutano huo umemalizika huku washiriki wakiahidi kutoa yuro milioni 414 kwa ajili ya usalama na ustawi wa eneo la Sahel na vilevile kulisaidia kundi la G-5 katika oparesheni zake.
Mkutano wa kimataifa wa misaada kwa eneo la Sahel barani Afrika umefanyika huku Afrika hususan nchi za eneo la Sahel zikikabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama na matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Umaskini mkubwa, matatizo ya chakula na mizozo ya kisiasa yote hayo yemekuwa yakizidisha wimbi la wahajiri kutoka eneo hilo, magendo ya binadamu, biashara ya madawa ya kulevya na harakati za makundi ya kigaidi katika eneo hilo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa pia imeyataja matatizo makubwa ya kiusalama huko magharibi na katika eneo la Sahel barani Afrika kuwa ni vitisho na mashambulizi ya makundi ya kigaidi, uhalifu wa kupangwa, magendo ya binadamu, silaha, biashara ya mihadarati na uporaji wa maliasili.
Katika upande mwingine hali ya kisiasa ya Libya na kutokuwepo serikali kuu nchini humo na vilevile kusambaratishwa kundi la kigaidi la Daesh huko Syria na Iraq na wakati huo huo kuwepo uwezekano wa kujipanga tena kundi hilo na kueneza ushawishi wake katika nchi mbalimbali kama zile za eneo la Sahel barani Afrika kumeifanya hali ya mambo ya eneo hilo kuwa tete zaidi. Kwa msingi huo nchi za eneo hilo zilikuwa zimeazimia kuanzisha kikosi cha wanajeshi wa kieneo kwa ajili ya kupambana na ugaidi na mpango huo umetekelezwa kwa uungaji mkono wa Ufaransa. Hata hivyo uhaba wa bajeti na kushindwa nchi nyingine za Ulaya kukidhaminia mahitaji ya fedha kikosi hicho kumechelewesha utekelezaji wa operesheni zake.
Baadhi ya matatizo ya Afrika kama wahajiri haramu wanaoelekea Ulaya, yanatishia usalama wa bara hilo kutokana na wimbi la ugaidi lililozikumba baadhi ya nchi za Ulaya. Kwa kutilia maanani hali hiyo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema kuwa: "Tunapasa kupambana na wahamiaji haramu na ni wazi kuwa suala hilo linahitaji kudhaminiwa usalama na kupatikana ustawi huko Afrika hususan katika eneo la Sahel.
Japokuwa nchi za Ulaya zimezungumzia ahadi zao za kifedha na suala la kuzisaidia nchi za Sahel huko Afrika, lakini inaonekana kwamba nchi hizo zinatumia kadhia hiyo kama wenzo wa kudhibiti wahajiri na kupambana na ugaidi kwa maslahi yao badala ya kijali na kutilia maanani utatuzi wa kimsingi wa matatizo ya migogoro ya Afrika.
Parstoday

No comments
Post a Comment