Writen by
sadataley
10:18 PM
-
0
Comments
Duru za serikali ya Somalia zimetangaza leo kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufuatia mlipuko wa jana wa bomu katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu imeongezeka na kufikia 45.
Afisa mmoja wa serikali ya Somalia ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa, watu 45 wamethibitishwa kufariki dunia hadi sasa na kwamba, waliojeruhiwa ni 36.
Wakati huo huo, afisa mmoja wa polisi ameziambia duru za habari kwamba, ana uhakika watu 36 wamepoteza maisha yao katika shambulio hilo la jana la kigaidi mjini Mogadishu.

Wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia
Ijumaa ya jana mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mawili yaliripuka sambamba na kujiri shambulizi la ufyatuaji risasi karibu na ikulu ya Rais Mohamedi Abdullahi Mohamed wa nchi hiyo na kusababisha hali ya mtafaruku.
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la al-Shabab limetangaza kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi ya jana. Licha ya wanachama wa kundi hilo kufurushwa kutoka katika maeneo muhimu ya taifa hilo la Pembe ya Afrika, lakini wanachama wake bado wanafanya mashambulizi ya kila mara dhidi ya taasisi za serikali na raia nchini humo.
Hadi sasa mapigano kati ya askari wa serikali ya Somalia wanaosaidiwa na askari wa Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, bado yanaendelea kushuhudiwa.
Somalia mbali na ukosefu wa usalama inakabiliwa pia na tatizo la uhaba wa chakuula kutokana na ukame unaoshuhudiwa katika nchi hiyo.
Parstoday

No comments
Post a Comment