Writen by
sadataley
9:51 AM
-
0
Comments
Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl, msanifu wa muungano wa Ujerumani mbili na mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika karne iliyopita, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 jana Ijumaa(16.06.2017).
Kansela Angeöla Merkel aliwaambia waandishi habari wakati akiwa katika ziarani mjini Rome kwamba Kohl ameonesha "uzalendo wa hali ya juu katika kuwahudumia wananchi pamoja na amani."
"Helmut Kohl kwa hiyo amekuwa mwale wa bahati kwetu sisi Wajerumani," amesema.
"Binafsi nafarijika kwamba alikuwapo," Merkel aliongeza, akisisitiza jukumu alilokuwa nalo katika kumsaidia kuingia katika siasa za mstari wa mbele. Kohl aliiongoza Ujerumani katika muungano mwaka 1990 na alikuwa kansela wa Ujerumani ya magharibi kuanzia mwaka 1982 hadi 1998 na kisha taifa la Ujerumani lililoungana .
Tangu pale alipoanguka na kupata athari katika ubongo mwaka 2008, Kohl amekuwa mgonjwa sana, hali yake ikiporomoka kwa kiasi kikubwa. Alikuwa yuko katika nyumba yake tu mjini Ludwigshafen, ambako alitembelewa mwezi Aprili 2016 na waziri mkuu wa hungary Viktor Orban .
Alifariki akiwa nyumbani kwake.
Viongozi mbali mbali duniani , viongozi wa zamani na wanasiasa walielezea hisia zao kutokana na kifo cha Helmut Kohl jana Ijumaa mara baada ya taarifa za kifo chake kupatikana.
Rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amesema " Wajerumani walimpa Helmut Kohl jina la utani "Kansela wa muungano." Hii ni sahihi na muafaka."
Viongozi watoa maelezo kuhusu Kohl
"Alitakiwa kujibu baadhi ya maswali mazito katika wakati wake, na katika kujibu kwa usahihi aliwezesha muungano wa Ujerumani iliyokuwa imara, yenye ufanisi na kuundwa kwa Umoja wa Ulaya."
"Msanifu wa muungano wa Ujerumani na urafiki kati ya Ujerumani na Ufaransa: kwa kifo cha Helmut Kohl , tumempoteza mtu muhimu sana katika Ulaya." amesema rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema, "Ni Mjerumani halisi na juu ya yote amefariki mtu halisi wa Ulaya."
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg , amesema "Kifo cha Helmut kinaniumiza sana. Mtu ninayejifunza kwake, rafiki wangu, mwenye uhalisia wa Ulaya, atakumbukwa sana, na tutamkosa sana."
"Helmut Kohl alikuwa sehemu ya Ujerumani iliyoungana katika Ulaya iliyoungana. Wakati ukuta wa Berlin ulipoanguka , alijitokeza juu kabisa. Mtu halisi wa Ulaya." Amesema waziri wa mambi ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel.
"Helmut alikuwa historia kubwa ya Ulaya. Alihakikisha muungano wa furaha kwa nchi yake na kusaidia ujenzi wa Ulaya na uhuru."
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amesema, "Kalale mahali pema Helmut Kohl, mtu mwenye maono katika Ulaya na kiongozi wa dunia. Katika enzi za kuongezeka kwa hali ya kujitenga tunaweza kujifunza mengi kutokana na mfanyo wame wa muungano."
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema, "kama kansela wa kwanza wa Ujerumani iliyoungana tangu mwaka 1945 alikuwa kinara wa historia ya ulaya. Kwa niaba ya watu wa Uingereza natoa hongera kwa jukumu alilochukua katika kusaidia kumaliza vita baridi na kuziunganisha Ujerumani mbili. Tumempoteza baba wa Ujerumani ya kisasa.
Waziri mkuu wa Italia Paolo Gentiloni amesema , Heko kwa kumbukumbu ya kansela Kohl. italia inamkumbuka kama muasisi wa muungano wa Ujerumani na kuanguka kwa ukuta katika bara la Ulaya."
DW Swahili
No comments
Post a Comment