Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 19, 2017

Umoja wa Afrika wazitaka Eritrea na Djibouti kuvumiliana

Ramani
Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU imeelezea wasiwasi mkubwa ilionao kutokana na kushadidi mvutano kati ya nchi jirani za Eritrea na Djibouti baada ya Qatar kuondoa askari wake waliokuwa wakisimamia amani katika maeneo ya mpakani yanayogombaniwa baina ya nchi mbili hizo za Kiafrika.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amezitaka Eritrea na Djibouti zijizuie na ziwe na uvimilivu katika kipindi hiki huku umoja huo ukitarajia kutuma timu maalumu ya uchunguzi kwa ajili ya kushughulikia mvutano baina ya nchi hizo.
Moussa Faki Mahamat amesema kuwa, hivi sasa lililo la msingi kwa nchi hizo ni kuwa na subira, kujizuia na kutochukua hatua yoyote itakayoshadidisha mvutano kati yao.
Mgogoro huo unaonekana kuchukua mkondo mpya baada ya Djibouti kuituhumu Eritrea kwamba, imezikalia kwa mabavu ardhi na maeneo yanayogombaniwa na nchi mbili hizo.
Qatar ilichukua hatua ya kuwaondoa askari wake wa kulinda amani kwenye mpaka unaozozaniwa na nchi mbili za Djibouti na Eritrea baada ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki kujiunga na kambi ya Saudi Arabia katika mgogoro ulioanzishwa na nchi hiyo na washirika wake dhidi ya Qatar. 
Serikali ya Doha ilikuwa imechukua pia nafasi ya upatanishi katika mzozo huo wa mpaka kati ya Djibouti na Eritrea.
Wakati huo huo nchi mbalimbali za kieneo na asasi tofauti ukiwemo Umoja wa Mataifa zimeendelea kuzitaka Eritrea na Djibouti kutochukua hatua yoyote ile itakayopelekea kushadidi mivutano kati ya nchi mbili hizo.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment