Writen by
sadataley
6:44 AM
-
0
Comments
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa
Francis amemtia moyo katika jitihada zake za kukabiliana na umasikini barani Afrika
pamoja na mabadiliko ya tabia nchi. Merkel amekutana na Papa Francis mjini Vatican jana
kwa dakika 40. Kansela ametangaza kuwa maendeleo ya Afrika yatakuwa ajenda kuu katika mkutano ujao wa kilele wa mataifa ya G20 mjini Hamburg, na kuongeza kuwa Francis ameupokea vyema uamuzi huo. Mkutano huo wa kilele vilevile unatarajiwa kulenga jitihada za kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi-kufuatia uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kujiondoa katika Makubaliano ya Tabia Nchi ya Paris, mwezi uliopita.
DW Swahili
No comments
Post a Comment