Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 17, 2017

Nikweli dili la Okwi, Simba limetiki

Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe (kulia) akiwa na Emmannuel Okwi.

Mshambuliaji Ibrahim Ajib yupo njiani kuelekea Yanga akitokea Simba, hiyo siyo habari nzuri kwa Wanasimba lakini kuna taarifa njema kwao.

Habari kutoka ndani ya Klabu ya Simba inaeleza kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za kumvalisha Emmannuel Okwi jezi namba 25 ambayo alikuwa kiitumia kikosini hapo kama usajili wake utakamilika.

Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, inadaiwa kuwa alitua jijini Dar es Salaam, jana usiku yupo katika mazungumzo ya mwishomwisho na klabu hiyo.

Kupitis ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Simba, ameweka picha ya Okwi akiwa na Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kisha kuandika ‘DEAL DONE’, ikionekana anamaanisha kila kitu kimekamilika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment