Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 21, 2017

Mfalme wa Saudi Arabia amtangaza mrithi wake

Naibu mwana mrithi wa Ufalme Saudi Arabia Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 amepandishwa cheo na kuwa mwana mrithi wa ufalme kuchukuwa nafasi ya binamu wake katika tangazo la ghafla Jumatano

Agizo la Ufalme limesema mwana mrithi wa ufalme Mohammed bin Nayef mkuu wa kupiga vita ugaidi anayehusundiwa na serikali ya Marekani kwa kuanzisha mashambulizi ya mabomu dhidi ya kundi la Al-Qaeda mwaka 2003 hadi mwaka 2006 ameondolewa katika nyadhifa zote na nafasi zake kuchukuliwa na Mohammed bin Salman ambaye anakuwa naibu waziri mkuu na kuendelea kushikilia nyadhifa za waziri wa ulinzi,mafuta na nyenginezo.

Uamuzi wa Mfalme Salman kumpandisha cheo mtoto wake huyo wa kiume na kuimarisha madaraka yake umeidhinishwa na wajumbe 31 kati ya 34 wa Baraza la Utii linaloundwa na wajumbe waandamizi wa familia tawala ya Al Saud kwa mujibu wa agizo la kifalme lililotangaza hayo.

Wachambuzi wanasema mabadiliko hayo yanamuwezesha mwana mfalme Mohammed bin Salman kuendelea haraka na mpango wake wa kupunguza utegemezi wa mafuta wa Saudi Arabia ikiwa ni pamoja na kubinafsisha kwa nusu kampuni ya mafuta ya taifa ya Aramco.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment