Akichangia mjadala huo wa bajeti, Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Ngwali (CUF) alisema wabunge warudi majimboni wakaombe radhi wananchi kwani wao ndiyo walipitisha sheria za madini.
“Tuliapa kwa kushika kurani na biblia, kurani na biblia ni vitabu vya Mwenyezi Mungu havitakiwi kudanganya, huwezi kuapa kisha ukazungumza uongo, unashika kurani ama biblia alafu ukaja kubadilisha ukazungumza mengine, kila siku tunasema tumerogwa na nani, tumerogwa na kurani na biblia.
“Mara nyingi ukiwa mkweli hukubaliki, kuna wakereketwa na wanaharakati walionesha hali ya madini ngumu, Dk. Hamisi Kigwangala ubunge wake ulikuwa wataabu kwa sababu alisimamia na kupinga madini haya yasiibwe hayachakachuliwi, alipigwa mabomu, aombwe radhi.
“David Kafulila ambaye alikuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) akaitwa tumbili, Zitto Kabwe alikuja na hoja nzito mwisho wa siku hapana ikawa ndio”alisema mbunge huyo.
No comments
Post a Comment